The House of Favourite Newspapers

Kikosi Cha Azam Kuhamia Kujiweka Sawa

AZAM (1)Wachezaji wa Azam wakifanya mazoezi.

Kikosi cha Azam FC, kesho kutwa Jumatano kinatarajiwa kwenda visiwani Zanzibar kuweka kambi ya muda mfupi ya kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuanza Desemba 17, mwaka huu.

Timu hiyo ambayo imemaliza mzunguko wa kwanza ikiwa nafasi ya tatu na pointi 25, imedhamiria kufanya kweli mzunguko wa pili huku ikifanya usajili wa maana kwa kuwanyakua Waghana watatu, Enock Atta Agyei, Yahaya Mohammed na Samuel Afful.

Meneja wa timu hiyo, Philip Alando, amesema leo Jumatatu kikosi chao rasmi kitaanza mazoezi huku keshokutwa Jumatano wakitarajiwa kwenda visiwani humo.
“Ni kweli tunaenda Zanzibar kama hakutakuwa na mabadiliko yoyote kwani kocha mkuu, Zeben Hernandez ndiye aliyepanga kambi iwe huko, hivyo kama akiendelea kushikilia msimamo wake huo, basi Jumatano tutapanda boti na tutakaa kwa siku tano mpaka kumi,” alisema Alando.

Comments are closed.