The House of Favourite Newspapers

Afisa Mkuu wa Polisi Kortini kwa Mauaji ya Mwandishi wa Habari

0

 OFISA Mkuu wa Polisi, Bi. Sabina Kerubo anatuhumiwa kuhusika na mauaji ya Mwandishi wa Habari wa The Star, Bw. Eric Oloo kutokana na mwili wa marehemu kukutwa nyumbani kwake mnamo Novemba 21, 2019.

 

Ofisa huyo alifikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Siaya, James On’gondo ambaye aliamuru kuwa Afisa huyo aendelee kuwa kizuizini Kituo cha Polisi cha Siaya kwa siku 14.

Katika hati ya kiapo, wapelelezi wanaoshughulikia kesi hiyo wameomba muda wa nyongeza wa kumshikilia Afisa huyo ili kumaliza uchunguzi juu ya mauaji hayo.

 

Aidha, wiki mbili zilizopita Mahakama iliamuru ndugu wawili, Victor Ogola Luta na Franklin Joel Luta, kukamatwa kwa ajili ya uchunguzi zaidi. Kesi hiyo itaanza kusikilizwa tena mnamo tarehe 10 Desemba mwaka huu.

Leave A Reply