The House of Favourite Newspapers

Agizo la Magufuli Lamtumbua Muonyesha Filamu

0

Tanzania's President elect John Pombe Magufuli addresses members of the ruling Chama Cha Mapinduzi Party (CCM) at the party's sub-head office on Lumumba road in Dar es Salaam, October 30, 2015. Tanzania's ruling party candidate, John Magufuli, was declared winner on Thursday of a presidential election, after the national electoral body dismissed opposition complaints about the process and a demand for a recount. The election has been the most hotly contested race in the more than half a century of rule by the Chama Cha Mapinduzi Party, which fielded Magufuli, 56, a minister for public works. REUTERS/Sadi SaidRais John Magufuli

Stori: Mwandishi Wetu, Risasi Jumamosi

DAR ES SALAAM: Kimenuka! Agizo la Rais John Magufuli la kuwataka watu kutotumia muda wa kazi kufanya starehe, limemtumbua kijana Mohamed Hamis (20) baada ya kukamatwa akiwa anaonyesha video kibandani, kazi iliyofanywa na Taasisi ya Haki Miliki (Cosota) hivi karibuni huko Temeke jijini Dar.

Tukio hilo lilitokea Mtaa wa Azimio Kaskazini, ambapo maofisa wa Cosota waliingia mitaani kusaka watu wanaokiuka agizo hilo, sambamba na kuwatafuta watu wanaoonyesha filamu pasipo kuwa na leseni.

Baada ya kukamatwa, kijana huyo alifikishwa kwa ofisi ya serikali ya mtaa ili wao waendelee na taratibu nyingine za kisheria dhidi yake.

Akizungumza na gazeti hili, mwenyekiti wa mtaa huo, Misheli Manyamba alikiri kutokea kwa tukio hilo na kudai mtuhumiwa huyo atafikishwa polisi na baadaye mahakamani.

“Ni kosa la kisheria kwa mtu yeyote kuonyesha filamu saa za kazi, anayekiuka agizo hilo ni lazima awajibishwe,” alisema mwenyekiti huyo.

Naye ofisa wa Cosota aliyejitambulisha kwa jina moja la Suleman, alisema wao kazi yao ni kusimamia sheria za nchi na agizo la rais lazima liheshimiwa kwa kijana huyo kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.

KUNUNUA NA KUSOMA MAGAZETI YA GLOBAL PUBLISHERS ONLINE, INGIA HAPA==>VODACOM M-PAPER APP

*********

JIUNGE NA SOCIAL MEDIA ZETU

KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA

INSTAGRAM: @Globalpublishers

ERIC SHIGONGO INSTAGRAM: @ericshigongo

TWITTER: @GlobalHabari

FACEBOOK: @GlobalPublishers

SUBSCRIBE YOU TUBE: Global TV Online

GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE:@shigongotz

Leave A Reply