The House of Favourite Newspapers

Ajali Yaua 1 Maeneo ya Mlimani City Dar

0

Ajali (1) Ajali (2) Ajali (3) Ajali (4) Ajali (5) Ajali (6)

Usiku wa kuamkia leo Agosti 19 maeneo ya mataa yaliyopo kati ya Mlimani City na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilitokea ajali mbaya ya gari ndogo ambayo haikuweza kufahamika kwa haraka kutokana na kugongwa na lori lililovuka na kuingia hadi kituo cha mafuta kilichopo jirani na mataa hayo.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo, gari ndogo ilikuwa ikiendeshwa na mwanamke ambaye mwili wake haukuweza kuokolewa kutokana na kubanwa.

Alipopigiwa simu ili kufafanua kama amepata taarifa za ajali hiyo, Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kinondoni amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa mtu mmoja ndiye aliyefariki na kueleza kuwa yupo kwenye kikao hivyo taarifa kamili ataitoa baadaye.

Leave A Reply