Ajali ya Ndege Yaua Watu 9 Marekani

WATU tisa wakiwemo watoto wawili wamefariki katika ajali ya ndege ndogo iliyotokea katika jimbo la Dakota ya kusini nchini Marekani.

 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na vyombo vya habari vya Marekani, ndege moja ndogo ilianguka muda mfupi baada ya kuruka. Tukio hilo lilitokea katika mji wa Chamberlain jimbo la Dakota ya Kusini.

 

Mamlaka zimefahamisha kwamba ndege hiyo ndege aina ya Pilatus PC-12 yenye mota moja ilikuwa imebeba watu 12. Katika ajali hiyo watu 9 wakiwemo watoto 2 walipoteza maisha. Watu 3 waliokolea wakiwa wamejeruhiwa.

 

Miongoni mwa waliofariki ni pamoja na rubani wa ndege hiyo. Hakuna taarifa rasmi iliyotolewa kuhusiana na chanzo cha ajali hiyo.


Loading...

Toa comment