The House of Favourite Newspapers

Ajib awafuata Messi, Suarez

0

Ibrahim-AjibMshambuliaji wa Simba, Ibrahim Ajib.

Hans Mloli,
Dar es Salaam
WAKATI bao la ‘kideo’ la mshambuliaji wa Simba, Ibrahim Ajib alilofunga juzi dhidi ya Mgambo likiendelea kuwa gumzo kwa wapenzi wa soka, mwenyewe amefunguka kuwa utundu huo ameupata kutokana na kutumia muda mitandaoni kuangalia video za wachezaji mahiri Ulaya; Lionel Messi na Luis Suarez wa Barcelona.
Ajib alifunga bao hilo kwa staili ya pekee baada ya kugongeana vizuri na Jonas Mkude na kufanikiwa kuwapiga chenga mabeki na kuingia ndani ya 18 kabla ya kumtisha kipa aliyelala chini kisha yeye ‘kuuchop’ mpira juu yake na kuzama wavuni, bao ambalo lilionyesha kuwakuna mashabiki waliokuwa uwanjani hapo.
Baada ya mchezo huo uliomalizika kwa Simba kushinda mabao 5-1, Ajib alisema: “Mpira ni kujifunza kila siku, najua lile bao zuri lakini siri ni kwamba nimekuwa nikiangalia sana wachezaji wakubwa wanafanya nini kila siku.
“Kina Messi, Suarez ni baadhi ya wachezaji ambao naangalia sana ‘clip’ za mabao yao, ndiyo matokeo yake haya.”

Leave A Reply