The House of Favourite Newspapers

Akutwa amechinjwa ndani ya mashine ya kusaga

1

Marehemu-Juma-Saidi-wa-kwanMarehemu Juma Saidi wa kwanza (kushoto) aliyevaa tishet iliyochanika akiwa na wenzake katika picha ya pamoja.

Na Johnson James,
IJUMAA GEITA:
Usiku wa kuamkia Januari 30, mwaka huu ulikuwa wenye huzuni na simanzi kubwa kwa familia ya Juma Said (35) kufuatia kuuawa kwa kuchinjwa na watu wasiojulikana.Tukio hilo la kinyama na lililowaumiza wananchi wengi, lilijiri kwenye Kitongoji cha Muungano wilayani Chato Mkoa wa Geita.

Chanzo kamili cha mtu huyo kuchinjwa hakijafahamika lakini Ijumaa kama kawaida yake lilifika eneo la tukio na kuzungumza na majirani, wafiwa, akiwemo mjane wa marehemu, Zawadi Msafiri ambaye ameachwa na watoto watatu.

SIKU YA TUKIO
Kwa mujibu wa majirani hao, usiku wa tukio, marehemu Juma alikuwa kwenye mashine ya kusaga nafaka akikoboa mpunga ambapo ndiyo ilikuwa kazi yake.
Majirani hao walisema kuwa, wakiwa wamelala walisikia mashine ikiunguruma lakini hawakujali kwa vile Juma alikuwa na kawaida ya kufanya kazi muda wowote.

mauaji30WANANCHI WAPISHANA LUGHA
Majirani hao walisema
kulipokucha walikwenda kuangalia kwenye mashine hiyo baada ya kuona imefungwa mpaka muda huo ndipo walipouona mwili wa Juma ukiwa sakafuni huku umelowa damu.

Baadhi ya watu waliamini kuwa, Juma alifariki dunia baada ya kujiweka mwenyewe kwenye mkanda wa mashine na kujimaliza lakini wengine walisema alichinjwa na wabaya wake kwa vile alikuwa akilala pale mashineni.

HOFU YA MAJIRANI
Majirani wenye makazi eneo hilo walisema kuwa, sasa wanaishi kwa woga wakiamini wanaweza kuvamiwa wakati wowote.

“Hawa waliomchinja shingo Juma hadi kufa hata sisi wanaweza kutuua. Tunasema Juma aliuawa kwa sababu yeye ndiye aliyekuwa na funguo za mashine lakini cha ajabu baada ya tukio, asubuhi milango ilikutwa imefungwa kwa nje.

“Tunaliomba Jeshi la Polisi Chato kuwasaka waliofanya kitendo hicho ili waweze kufikishwa mahakamani,” alisema jirani mmoja bila kutaja jina lake.

Mke wa Marehemu Juma akiwa na watoto wakeMke wa Marehemu Juma akiwa na watoto wake.

BOSI WAKE ATOA NENO
Jamila Abdul ni bosi wa marehemu Juma kwani ndiye mmiliki wa mashine hiyo. Anasema:
“Mimi nimefanya kazi na Juma kwa miaka 7 sasa tangu nilipompokea. Hivi karibuni alimkimbia mkewe mkubwa aliyejulikana kwa jina la mama Magreth ambapo Juma alikuwa amejenga nyumba lakini kutokana na kutoelewana na mke wake huyo ikambidi aukimbie mji na kuja kufanya kazi hapa kwangu.

“Lakini kila siku alikuwa akiniambia kuwa, mkewe huyo wa zamani anamsumbua. Ikafika hatua akasema anataka kujiua, mimi nikamwambia aache kwani kufa ni mipango ya Mungu. Jana jioni (Januari 29) nilikuwa naye majira ya saa moja na nusu jioni niliposikia amechinjwa nilishangaa sana.”

MKE MKUBWA ADAI MALI KWENYE MAZISHI
Baada ya mauti kumkuta Juma, aliyekuwa mke wake huyo ambaye walitengana miaka nane iliyopita wakiwa wamefanikiwa kupata mtoto mmoja, aliishangaza jamii pale marehemu alipopelekwa Kijiji cha Kanyange nje kidogo ya mji wa Chato kwa mazishi ambapo yeye alianza kudai mali.

Familia ya mke wa Juma wakiwa msibani.

Familia ya mke wa Juma wakiwa msibani.

Mwanamke huyo alisema anataka mali ambazo marehemu alizipata alipokuwa akifanya kazi kwa Jamila. Hata hivyo, wazee wa kimila walimkoromea na kumtaka aache kudai mali hizo.
Naye mke mdogo wa marehemu alipozungumza na Ijumaa alisema ameumizwa na kifo cha mumewe kwani amemuacha na watoto watatu.

“Mimi na mume wangu tulikuwa tukiishi vizuri. Ila baadhi ya siku nilizokuwa nikipigizana naye keleke ni kuhusu ulevi.

Alikuwa mlevi wa kupindukia hivyo nilikuwa naongea naye na kuniahidi ataacha. Kuhusu kulala mashineni ni kweli, lakini ni kama mlinzi baada ya mlinzi aliyekuwa analinda pale kuacha kazi na kuhama kabisa eneo hili,” alisema mwanamke huyo.

HISTORIA FUPI YA MAREHEMU
Marehemu ambaye alizaliwa wilayani Kahama mkoani Shinyanga kisha kupata pigo kwa baba yake mzazi kufariki dunia akiwa na umri wa miaka 3, alikulia kwa dada yake ambaye alikuwa akiishi Nyakabango mpaka alipooa na kujenga nyumba yake mwenyewe.

KAMANDA WA POLISI
Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, ACP Lotson Mponjoli amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa, uchunguzi wa kubaini chanzo cha tukio hilo unaendelea na muda ukifika atatoa matokeo.

1 Comment
  1. Rose Maleko says

    Inasikitisha shana.

Leave A Reply