The House of Favourite Newspapers

Ali Kiba amdatisha Niyonzima

0

Kiba.jpgAli Kiba

Wilbert Molandi,

Dar es Salaam

KIUNGO mchezeshaji wa Yanga Mnyarwanda, Haruna Niyonzima amemtaja mkali wa Bongo Fleva, Ali Kiba ‘kuwa ndiye anayemzimia nchini.

Kauli hiyo, aliitoa katika uzinduzi wa video ya wimbo wake mpya wa Lupela hivi karibuni jijini Dar es Salaam.

NIYONZIMANEW4Kiungo mchezeshaji wa Yanga Mnyarwanda, Haruna Niyonzima

Akizungumza na Championi Jumatano, Niyonzima alisema kuwa, tofauti na kumkubali kwa uwezo wake wa kuimba, pia ni rafiki wake wa karibu wanayekutana na kujadiliana masuala mbalimbali ya kimaendeleo.

“Kwa hapa Tanzania wasanii wengi nawakubali kwa kusikiliza nyimbo zao pekee, lakini siyo kwa Kiba yeye ninampenda kwa nyimbo zake na hata yeye mwenyewe kutokana na ukaribu niliokuwa nao na mara nyingi nimekuwa nikienda kwenye shoo zake.

“Mimi kila wakati ninazungumza na Kiba kwa kukutana na kuzungumza katika simu katika masuala ya maendeleo ya muziki na hata soka, hivyo ni mtu wangu wa karibu, tulijuana na kuzoeana baada ya mimi kupenda kazi yake ya muziki,” alisema Niyonzima.

Leave A Reply