The House of Favourite Newspapers

Amissi Tambwe hizi sasa dharau

0

STRAIKA wa Yanga, Amissi Tambwe amewata mashabiki wa timu yake kutulia na kutohofia lolote katika mechi ya leo ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba, kwani ni ya kawaida kama ile ya JKT Ruvu waliyoshinda mabao 4-1.

Homa ya mechi hii ya watani imepanda kwa mashabiki wa timu zote mbili lakini Tambwe aliyewahi kuichezea Simba amelimbia Championi Jumamosi kuwa; “Mashabiki wa Yanga watulie waone tutafanya nini.”

Tambwe raia wa Burundi alisema haoni kitu cha kumuumiza kichwa katika mchezo huo anachofikiria ni kuendeleza rekodi ya ushindi katika mechi za ligi kuu.

“Simba ni timu ya kawaida tu kama zilivyo timu nyingine, yaani kama JKT Ruvu tuliyoifunga mabao 4-1, hivyo hata Simba tunaweza kuifunga mabao hayo kwani ni ya kawaida,” alisema Tambwe.

“Haina haja ya mashabiki wa Yanga kuogopa labda kuja uwanjani au vinginevyo, nasema waje waone tunavyorejesha heshima ya timu yetu kwa Simba.”

Hii ni mechi ya pili kwa Tambwe kuichezea Yanga dhidi ya Simba tangu alipojiunga nayo Desemba mwaka jana akitokea Simba ambako aliachwa saa chache kabla ya dirisha la usajili kufungwa.

Leave A Reply