The House of Favourite Newspapers

Anayedaiwa baunsa Yamoto Band asakwa kwa mauaji ya mchumba’ke!

0

bunsa yamoto (8) Kassim Said ‘Baunsa Rambo’ na marehemu.

Stori: Dustan Shekidele, Risasi Jumamosi

MOROGORO: Kijana aliyefahamika kwa jina la Kassim Said ‘Baunsa Rambo’ mkazi wa jijini Dar ambaye inadaiwa ni mmoja wa mabaunsa wa Bendi ya Yamoto, anasakwa na polisi kwa madai ya kuhusika na mauaji ya mchumba wake aitwaye Mwajabu Ibrahim.

bunsa yamoto (7)Waombolezaji wakiwa msibani.

Tukio hilo lilitokea Jumapili iliyopita ambapo inadaiwa kuwa, Kassim alimshushia kipigo Mwajabu baada ya kutofautiana kabla ya kesho yake mwanamke huyo kukutwa akiwa amekufa chumbani kwake.

bunsa yamoto (1)Chanzo chetu cha kuaminika kilidai kuwa, awali wawili hao walianza kuzinguana walipokuwa kwenye grosari anayomiliki Mwajabu iliyopo Mtaa wa Kilosa ambapo kijana huyo alimpiga mwezake kabla ya watu kuwaamulia.

bunsa yamoto (9)Jeneza lenye nmwili wa marehemu.

“Hatukujua kilichoendelea baada ya ugomvi ule mpaka kesho yake tulipopata taarifa kuwa Mwajabu kakutwa amekufa. Kuna mwanaye anaitwa Fatuma, yeye atakuwa na siri ya tukio hilo,” alisema mtoa habari huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake.

bunsa yamoto (5)Baba wa marehemu

Kufuatia taarifa hiyo, mwandishi wetu alifunga safari hadi Mtaa wa Kilosa Town Kata ya Mkwatani na kubahatika kuongea na mtoto wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Fatuma Mayuwe ambaye alisema:

bunsa yamoto (10)“Siku ya tukio (Jumapili) Kassim Rambo anayefanya kazi Bendi ya Yamoto alikuja hapa kwenye grosari ya mama, mara akamnyang’anya mama simu na kuanza kuipekua huku akimtuhumu kuchepuka.

“Sasa sijui aliona nini kwenye simu, ghafla nikaona anampiga mpaka akatapika damu, watu wakawaamulia na hali ya amani ikarejea.

bunsa yamoto (11)“Usiku mama na Kassim wakaniaga kuwa wanakwenda kwenye shoo ya Mashauzi, mimi na mdogo wangu tukalala kwenye chumba chetu nao wakafunga chumba chao wakaondoka, cha ajabu asubuhi tumekuta mama amekufa kwenye chumba chake huku akiwa mtupu,” alisema Fatuma kisha akaanza kuangua kilio.

bunsa yamoto (12)Naye baba wa marehemu aliyefahamika kwa jina la lbrahim Mayuwe alipozungumza na gazeti hili alisema: “Mwanangu miezi kadhaa iliyopita alinieleza kuwa amepata mchumba mkazi wa Dar na anafanya kazi pamoja na Bendi ya Yamoto.

bunsa yamoto (2)Shughuli ya mazishi

“Siku chache baadaye kijana huyo ambaye ni Kassim alikuja na mshenga kukamilisha taratibu zote za ndoa na tulichokuwa tunasubiri ni ndoa tu.

bunsa yamoto (6)Mtoto wa marehemu

“Cha kusikitisha ni kwamba juzi walipokuwa wanatoka kwenye Taarab zao, kamfanyia ukatili na mwanangu amekufa. Taarifa zimefika polisi katika Kituo cha Kilosa na bado anasakwa kwa mauaji hayo,” alisema mzee huyo huku akilengwa na machozi.

Kufuatia Kassim kudaiwa kuwa ni mmoja wa mabaunsa wa Bendi ya Yamoto, mwandishi wetu aliwasiliana na Meneja wa bendi hiyo, Saidi Fella ambapo alipoulizwa kama anamjua kijana huyo alisema:

bunsa yamoto (4)Mtuhumiwa

“Huyo baunsa siyo wa kwetu, hata mimi nimeshapigiwa sana simu kuhusu hilo suala, sisi baunsa wetu anaitwa Mzungu, anakaa Temeke, huyo labda atakuwa huwa anatumika kwenye shoo za bendi mbalimbali.”

bunsa yamoto (3)Hata hivyo, mmoja wa viongozi wa bendi moja ya Taarab ya jijini Dar aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema kuwa anavyojua Kassim mara kadhaa amewahi kwenda Kilosa na Bendi ya Yamoto, lakini baunsa huyo pia alishawahi kufanya kazi na Mashauzi Classic.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Ulrich Matei hakuweza kupatikana mara moja kuzungumzia tukio hilo ila mmoja wa maafisa wa polisi aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema kuwa, Kassim anasakwa akihusishwa na mauaji hayo.

Leave A Reply