Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Lameck Nchemba hivi karibuni akiwa ziarani mkoani Mtwara alizungumza na Askari wa Jeshi la Magereza Mkoani humo na kusema kuwa CHADEMA wasithubutu kuandamana kwani kwa kufanya hivyo si kuwa watakuwa wanatingisha kiberiti cha njiti, bali watakuwa wanachezea gesi. Amesema kuwa sio kila kitu mtu anatakiwa kujaribu kwa sababu vingine huenda vikakuumiza.
MWIGULU AKIZUNGUMZA
Pia Waziri Mwigulu aliwataka Jeshi la Polisi kuhakikisha wanaanza kuwakamata wote wanaoagiza kufanyika maandamano nchi nzima.
Waziri aliyasema maneno hayo akiwaasa viongozi wa CHADEMA kutupilia mbali mpango wa maandamano na mikutano ya siasa nchi nzima Septemba Mosi mwaka huu.
Kufuatia kauli hiyo ya Waziri Mwigulu Lameck Nchemba, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema) amemjibu wakati akizungumza kwenye kikao cha ndani cha chama hicho.
Msikilize hapa.
Global Publishers and General Enterprises Limited is a registered private company dealing in publishing of weekly Swahili newspapers in Tanzania, namely; Uwazi, Ijumaa, Championi, Amani, Risasi & Ijumaa Wikienda.