The House of Favourite Newspapers

Ayoub Semtawa… Dakta ri anayeki piga Coastal Union

0

MOJA ya kasoro kubwa za wanasoka wengi hapa nchini na duniani kote ni elimu. Wanasoka wengi wamekuwa na elimu za kawaida hasa zile za sekondari na ni nadra sana kumuona mchezaji akiwa na elimu kubwa kama stashahada (diploma) au shahada (degree).

 

Lakini hilo ni tofauti na ilivyo kwa kiungo wa Coastal Union ya Tanga, Ayoub Idrisa Semtawa ambaye amebukua kwa kupiga kitabu kinoma na amechukua Shahada ya Utabibu katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).

 

Elimu yake ilipoanzia

Kiungo huyu ambaye amewahi kuichezea Mtibwa Sugar ya Morogoro, alianza elimu yake katika Shule ya Msingi Maendeleo wilayani Kilombero, mkoani Morogoro.

 

Kisha akajiunga na Sekondari ya Magila, Muheza mkoani Tanga alikosoma hadi Kidato cha Nne na hakuishia hapo kwani alihamia Muheza High School alikosoma hadi Kidato cha Sita kabla ya kujiunga na MUHAS.

 

Amewezaje kumudu soka na kusoma?

Semtawa anasema: “Napanga mambo yangu kwa wakati, wakati wa kusoma ni wa kusoma na soka pia lina wakati wake.

 

“Uzuri ni kuwa soka ni mchezo wa wakati fulani katika siku, hauchukui siku nzima.

Siku zote, nimeweza kufanya mazoezi na kuingia darasani kusoma bila matatizo.”

 

Malengo yake ni yapi?

Kiungo huyo anafunguka kuwa kitu anachokitamani ni kuona anaendelea kusoma kwa kiwango kikubwa katika fani yake hiyo.

 

“Nataka kuona nasoma zaidi katika fani hii, nataka kusoma kwa kiwango cha juu zaidi.

 

Lini atajikita zaidi kwenye fani yake?

Kiungo huyo anasema kuwa mara baada ya kustaafu soka ndiyo atajikita zaidi katika masuala ya udaktari ambao ameusomea.

 

“Kama nitafanikiwa kupata maendeleo mazuri katika soka, nitaelekeza nguvu zangu zaidi kwenye soka, kwa maana nikipata timu itakayonipa maslahi mazuri, lakini kama sikupata bahati hiyo, basi mapema tu nitaelekeza nguvu zangu kwenye kazi yangu na soka nitacheza kujifurahisha tu.

 

Changamoto alizokutana nazo

“Changamoto ni sehemu yoyote ile, hakuna kitu ambacho kinafanyika bila ya kuwa na changamoto.

 

“Kitu kikubwa ni kupambana kuona kwamba unakamilisha kitu ambacho umekipanga, ukifanya hivyo kila kitu kinaenda sawa kama vile ambavyo umepanga.

 

Mipango yake katika soka

“Hakuna ambaye hana mipango mikubwa katika soka, natamani kuona nacheza kwa levo kubwa zaidi ya hapa nilipofika kwa sasa.

“Natamani kufika mbali ikiwezekana hata nje ya nchi, huko ndipo ambapo nafikiria kucheza.”

 

Alipotokea Kiungo huyo awali alianza kuonekana kwenye ligi akiwa na klabu hii ya Coastal Union baada ya kupandishwa kutoka timu B aliyojiunga nayo mwaka 2012 baada ya kufanya vizuri katika mechi za timu hiyo.

 

Pia kwa nyakati tofauti amewahi kuzichezea timu za Vagarant ya Kilombero, Fish Stars na Bambino za Muheza.

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Leave A Reply