Azam Chupuchupu Kuchezea Kichapo

KLABU ya Azam jana iliponea chupuchupu kupokea kichapo mbele ya JKT Tanzania na kulazimishwa sare ya mabao 2-2 katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, uliopo Chamazi, Dar.

 

JKT walikuwa wa kwanza kupata bao likifungwa dakika ya 12 kipindi cha kwanza kupitia kwa Edward Songo, kisha Azam kujibu mapigo kupitia kwa Aggrey Morice dakika ya 78 kipindi cha pili.

 

JKT walirudi tena mchezoni na kupata bao la pili likifungwa na Danny Lyanda dakika ya 85 baada ya kutokea kona, huku Idd Seleman ‘Nado’ akiisawazishia Azam katika dakka ya 88.

 

Kwa matokeo hayo Azam FC wanafikisha pointi 20 sawa na Tanzania Prisons, ambao wapo nafasi ya tatu, huku Azam ikiendelea kubaki nafasi ya nne kutokana na utofauti wa mabao na Prisons waliopo nafasi ya tatu.

ISSA LIPONDA, Dar es Salaam


Loading...

Toa comment