The House of Favourite Newspapers

Baada ya Uchaguzi wa Umeya Kuvunjika, Chadema Kwenda Mahakamani Kudai Haki

cdm
“CHADEMA ilianzisha Operesheni Umoja wa Kupambana Udikteta Tanzania (UKUTA), hatuwezi kukaa kimya tena, Nyerere alikataza Vijana kuwa wanyonge na waoga, hakutaka Taifa la watu waoga, na sisi tunasema mwisho wa uoga umekwisha, tutakwenda Mahakamani kwa sababu kilichotokea leo kwenye Uchaguzi wa Meya wa Manispaa Kinondoni leo ni uhuni, kanuni na taratibu zinavunjwa waziwazi”

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa CHADEMA Taifa, Dkt. Vincent Mashinji, wakati akiongea na waandishi wa habari Makao Makuu ya Chama hicho yaliyopo Kinondoni jijini Dar es salaam, leo Jumapili 23/10/2016 baada ya Uchaguzi wa kumapata Meya wa Manispaa ya Kinondoni kuvunjika.

Wanatumia vyombo vya dola kudhibiti, Polisi kwenye uchaguzi wamekuwa wengi kuliko wajumbe ili wawatie hofu wajumbe na wananchi waliojitokeza kushuhudia Uchaguzi huo, Polisi wamewazuia kuingia ndani Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mhe. Freeman Mbowe na Katibu Mkuu wa CHADEMA kushuhudia Uchaguzi huo, vyombo vya habari vinavyoripoti bila kupendelea upande wowote vimezuliwa kuingia, waliozuiwa kuingia ni mwandishi wa Mwananchi, Mtanzania na Tanzania Daima, huku wakiruhusu waandishi wao wa TBC, Uhuru na Mzalendo, unaweza ukaona jinsi nchi inavyoendeshwa na Serikali ya awamu ya tano.

CHADEMA kimesema hakitakuwa Chama cha kulalamika tena, watakwenda Mahakamani, watakusanya ushahidi na kudai haki, Mashinji amesema wameanza kudai Katiba ya Wananchi ndiyo suluhisho ya kila kitu, ni Katiba ambayo ni ya Wananchi ambayo ikipatikana mambo kama haya ya uvunjaji Sheria,kanuni na taratibu katika nchi utakwisha.

Madiwani wa Ukawa walitoka nje ya ukumbi wa kupigia kura mara baada ya kubainika mbinu chafu zilizokuwa zimeandaliwa ili mshindi atoke CCM, Wajumbe kutoka nje ya Manispaa ya Kinondoni wameingizwa kwenye Uchaguzi huo ikiwa ni kinyume na Sheria na taratibu, huku wajumbe halali wa UKAWA wakitolewa kushiriki Uchaguzi huo, waliotolewa ni Mhe. Susan Lyimo na Salma Mwasa.

Akiongea Mhe. Halima Mdee amesema watakwenda Mahakamani kwa kuwa ni ukiukwaji wa sheria, taarifa ya Uchaguzi hutolewa ndani ya siku 7, ili kutafuta wajumbe, kuangalia mkinzano wa kisheria ili mambo yawekwe sawa, lakini kilichofanyika taarifa imetolewa siku 1 kabla ya Uchaguzi ili wafanye mbinu zao ovu, Madiwani wapo 34, ili akidi itimie lazima kura zipigwe 23,lakini wamepiga kura wajumbe 18 tu, huo ni uvunjaji wa Sheria ndo maana CHADEMA imeamua kwenda mahakamani.

Comments are closed.