The House of Favourite Newspapers

Bahanuzi atoa onyo kali Ligi Kuu Bara

0

IMG-20120730-00024Ibrahim Mussa, Dar es Salaam
LICHA ya kufunga mabao matatu tu tangu msimu huu uanze, straika wa Mtibwa Sugar, Said Bahanuzi, amejipanga kurudisha makali yake ya kucheka na nyavu mara tu Ligi Kuu Bara itakapoendelea Desemba 12, mwaka huu.

Mtibwa Sugar ambayo inashika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 22, imecheza michezo tisa huku ikibakiwa na michezo sita kuhitimisha mzunguko wa kwanza.

Akizungumza na Championi Jumatano, Bahanuzi alisema kuwa kila kitu kinakuja kwa wakati hivyo amejipanga vizuri kuhakikisha anafunga mabao ya kutosha katika michezo iliyobakia.

“Unajua suala la ufungaji kwa mchezaji ni kitu cha kawaida kwa sababu linaongeza changamoto ya kuisadia timu ila jambo la msingi kwa sasa ni kujipanga na kufanya mazoezi kwa bidii maana naamini kila kitu kinawezekana, siwezi kukata tamaa.

“Kitu cha kwanza ambacho ni muhimu kwangu ni lazima nijitoe kwa nguvu zote kuhakikisha naisaidia timu yangu inafanya vizuri katika mechi sita zilizobaki kabla ya mzunguko wa pili haujaanza kwani itakuwa rahisi sana kwangu kutimiza kile ambacho nimepanga kukifanya msimu huu,” alisema Bahanuzi.

Leave A Reply