The House of Favourite Newspapers

Barcelona yavunja Mkataba na Guardiola

0

Rescissione-Sergi-GuardiolaSergi Guardiola.

Barcelona, Hispania

KLABU ya Barcelona nchini Hispania imeingia kwenye headline leo baada ya kuvunja mkataba wake na mchezaji Sergi Guardiola saa moja tu baada ya kumsajili.

Hii imetokea baada ya Sergi Guardiola (hana uhusiano na kocha Pep Guardiola) kuandika kwenye mtandao wa twitter maneno ambayo yanaonesha kuuchukiza uongozi wa Barca.

Maneno aliyoandika Sergi mtandaoni: dating back to 2013

SERGI_GUARDIOLA_GETAFEKiungo Guardiola mwenye umri wa miaka 24, kabla ya kujiunga na Barca alikuwa akichezea timu ya Alcorcon inayoshiriki ligi ndogo za Hispania.

Walichokisema Barca  kuhusu Guardiola ni hiki hapa.

FC Barcelona imeamua kuvunja mkataba wake iliosaini na Sergi Guardiola ambaye pia aliingizwa kwenye kikosi B cha Barcelona, baada kugundua kuwa ameandika kwenye mtandao wa twitter maneno yanayolenga kuichafua klabu ya Barca and Catalonia.

Sergi alipohojiwa na kituo cha redio cha Cope nchini humo alisema: “Nafahamu nimetanda kosa. Naomba msamaha kwa Catalonia and Barcelona. Nafahamu maamuzi yaliyofikiwa dhidi yangu”.

“Nataka niweke wazi kwamba. Hayo maneno yaliyozagaa kwenye twitter sikuandika mimi, bali ni rafiki yangu ndiye aliyechukua suimu yangu na kufanya hivyo. Tumeshindwa kuelewana. Tweet ni ya kuanzia mwaka 2013, ni matani tu ya rafiki yangu, sikufahamu kabisa kama kuna tweet ameiweka mtandaoni inayonihusu mimi.

Leave A Reply