The House of Favourite Newspapers

Ben Ali: Rais Aliyehukumiwa Kufungwa Maisha Mara Mbili

ZINE EL ABIDINE ALI  alikuwa mwanasiasa wa Tunisia ambaye aliongoza kama rais wa nchi hiyo kwa miaka 23, kuanzia mwaka 1987 mpaka alipoondolewa madarakani mwaka 2011.

Januari 14 mwaka 2011, mwezi mmoja baada ya maandamano ya kupinga uongozi wake, Ben Ali na familia yake walitimkia Saudi Arabia ambako wamekuwepo mpaka aliporipotiwa kufariki jana. Serikali ya Tunisia iliwaomba polisi wa kimataifa (Interpol) kumkamata marehemu Ben Ali kwa makosa ya utakatishaji wa pesa na biashara ya madawa ya kulevya.

 

Ali na mkewe, Leila, waliwahi kupata misukosuko kibao kutokana na wizi na matumizi mabaya ya sheria na wakahukumiwa kwenda jela, ambapo rais huyo wa zamani aliwahi kuhukumiwa vifungo viwili vya maisha jela ambavyo hakuvitumikia kikamilifu katika mazingira yaliyokuwa nchini humo.

 

Februari 17 2011, iliripotiwa alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya kupooza na amekuwa akipata matibabu kwa muda mrefu, taarifa ambazo mwanasheria wake alizikanusha na kudai kuwa Ali alikuwa kwenye hali ya kawaida.

Ben Ali amefariki Septemba 19 mjini  Jeddah, Saudi Arabia, akiwa na umri wa miaka 83.

 

Comments are closed.