The House of Favourite Newspapers

Bendi kongwe kufunika Valentine’s Day Dar Live

0

Twanga (6)Mwandishi Wetu,

Dar es SalaamBENDI kongwe za muziki wa dansi nchini, The African Stars ‘ Twanga Pepeta,’ Sikinde, Msondo Ngoma na Kundi la Muziki wa Taarab la Tanzania One Theatre (TOT), chini ya Khadija Kopa, zinatarajiwa kufunika Februari 14 katika siku ya wapendanao, Valentine’s Day ndani ya Ukumbi wa Dar Live, Mbagala-Zakhem jijini Dar.

Akizungumza na mtandao huu, Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo, alisema siku hiyo ambayo ni maalum kwa wapendanao duniani kote, Dar Live, imeamua kuwaletea kitu cha tofauti.

“Njoo ukiwa umependeza na mwandani wako mcheze na kuimba muziki mzuri kutoka kwa wakongwe wa Muziki wa Dansi. Niwaahidi tu Dar Live tumewaandalia zawadi maalum wale wote watakaopendeza, kucheza na kuimba vizuri sambamba nyimbo za Sikinde, TOT, Msondo na Twanga Pepeta,” alisema Mbizo.

Aidha, Mbizo alimalizia kwa kutaja viiingilio vya siku hiyo muhimu kuwa vitaanzia Sh 1,000 kwa kawaida na Sh 20,000 kwa VIP, lakini mapema kutakuwa na burudani na michezo ya watoto mpaka saa 12 jioni kwa kiingilio cha Sh 2,000 tu.

Leave A Reply