The House of Favourite Newspapers

Beyonce atumbua jipu

0

Beyonce-Knowles-Cosmopolitan-UK-2
DIVA wa muziki wa Pop, Beyoncé Knowlese.

DIVA wa muziki wa Pop, Beyoncé Knowlese ameamua kubadilisha menejimenti yake baada ya kumtimua meneja wake wa biashara aliyedumu naye kwa muda mrefu na kuajiri timu mpya kwa ajili ya kumsogeza mbele zaidi.

Kupitia mtandao wa Page Six umedai kuwa, Beyoncé amevunja mkataba na meneja wake wa miaka mitano, Lee Anne Callahan-Longo na kwa sasa anafanya kazi na Steve Pamon aliyekuwa mkuu wa masoko kwa upande wa michezo na burudani wa benki ya JPMorgan aliyesaidia benki hiyo kutoa udhamini kwa ziara yake ya On the Run.

Mtandao huo ulienda mbali zaidi na kudai kuwa Beyoncé ametimua timu nzima ikiwa ni pamoja na binamu yake. Beyoncé alimchukua Pamon kusimamia kampuni yake ya Parkwood Entertainment inayofanya kazi ya usimamizi, utengenezaji muziki, ziara, picha na kazi zingine.

(Imeandaliwa na Andrew Carlos/GPL)

Leave A Reply