The House of Favourite Newspapers

Bifu Za Mastaa Bongo… Zilizoacha Historia

0

Makala: Chande Abdallah
Ukiacha bifu nzito zilizotikisa dunia mpaka kusababisha vifo vya mastaa wakubwa kama Notorious BIG na Tupac, zifuatazo ni orodha ya bifu zilizotikisa kwenye tasnia ya muziki Kibongobongo na kuacha historia kubwa kiasi kwamba hata mastaa hao walivyopatana mashabiki wao walibaki vinywa wazi kwa kutoamini kilichotokea.

Ali ChockVs Asha BarakaAllyChokinew

Ali Chockasha

Asha Baraka

Bifu lao lilianza baada ya kuhitilafiana kwenye uhamisho wa mpiga gitaa wa Twanga Pepeta, Shakashia ambapo Asha Baraka akaanza kudai gari alilomnunulia Chocky na kufikishana mahakamani ambapo bifu lao likazidi kushika kasi kiasi cha kuapiana kutozikana.

Hata hivyo, wawili hawa walimaliza bifu lao na kukumbatiana ndani ya Studio za Global TV Online zilizopo Bamaga-Mwenge.

Dudu Baya Vs Mr Nicedudu baya

Dudu Baya

nice5Mr Nice

Wawili hawa walionesha kuwa na bifu zito baada ya Dudu Baya kumtwanga makonde Mr Nice mbele ya mashabiki wake na kufikishana mahakamani ambapo Dudu baya aliswekwa rumande. Hata hivyo, wawili hao katikati ya mwaka jana walimaliza tofauti zao huku picha yao wakiwa pamoja ikizua gumzo kwenye mitandao kibao Bongo.

Tid Vs Q–Chillah tid (1)

Tid

chillaQ–Chillah

Wawili hawa waliungana na kutengeneza bendi waliyoiita Top Band na kufanya ngoma kali ya Nilikataa, lakini baadaye wakafarakana na kila mmoja akawa kivyake huku wakirushiana maneno kila mara, mwaka 2015 wakongwe hawa walipatanishwa na kuahidi kufanya kolabo ya pamoja ili kuwaonesha mashabiki wao kama wamepatana.

Matonya Vs Tunda Manmatonya

Matonya

TUNDA

Tunda Man

Bifu hili lilikuwa ghafla wakati huo Matonya ndiyo alikuwa hot ambapo Tunda Man aliibua madai ya kumtungia nyimbo kibao Matonya ikiwa ni pamoja ya Vaileti jambo ambalo Matonya alilipinga na kusababisha bifu zito baina yao, hata hivyo bifu hilo lilisuluhishwa kwenye vyombo vya habari na kuisha mwishoni mwa mwaka 2015 kwa wawili hao kufanya wimbo wa pamoja unaokwenda kwa jina la Ugomvi.

Bob Junior Vs Diamonddiamond-platnumz

Diamond

bob_junior_sharobaro2
Bob Junior

Bob Junior ambaye ni prodyuza aliyemtambulisha Diamond kwenye gemu, aliingia bifu na msanii huyo kiasi cha kuacha kufanya kazi pamoja na bifu hilo likikolezwa na vita ya nani Rais wa Sharobaro huku ikidaiwa kuwa na figisufigisu nyingizi mbali na sababu hiyo. Hata hivyo, wawili hawa walionesha kumaliza tofauti zao na katika shoo ya Zari All White Party iliyofanyika Mei mwaka jana ambayo ilimuhusisha mwandani wa Diamond, Bob Junior alijumuika nao na kufurahi pamoja kuonesha kuwa hawana bifu tena.

Nay wa Mitego Vs Madeenay

Nay wa Mitego

 

 

Madee2

Madee

Bifu la wakali hawa lilianza kama utani kwa kugombania hadhi ya Rais wa Mazense ambapo kila mmoja alidai kuwa na haki hiyo kiasi cha wawili hao kutajwa kufanyiana fujo hata kwenye shoo. Hata hivyo, walipatana mwaka 2014 na kuwashangaza watu kwa kupeana lifti na kupiga picha wakiwa kwenye gari moja.

Bifu nyingine ambazo nazo zilitikisa na kuacha historia lakini zilikuja kusuluhisha ni pamoja na Nasma Kadogo na Khadija Kopa, Inspector Haroun na Juma Nature, O’Ten vs Afande Sele na nyingine nyingi.

Leave A Reply