The House of Favourite Newspapers

Bodaboda yamponza Bond

0

bondNa Gladness Mallya, RISASI MCHANGANYIKO

Kitendo cha msanii wa filamu Bongo, Bond Suleiman kutumia usafiri wa bodaboda kutoka Dar hadi Shinyanga kuwahi kumuuguza baba yake mzazi kimemponza.

Akipiga stori na Za Motomoto News, Bond alisema baada ya kufika kwao kwa kutumia usafiri huo licha ya baba yake kuwa hoi, alimjia juu na kumkanya asirudie tena kwani alitoka Dar saa sita usiku na kufika saa 12 jioni ya kesho yake jambo ambalo ni hatari.

“Siyo baba tu aliyekasirika hata majirani hawakupendezwa, sitasafiri tena na chombo hiki umbali mrefu, nilifanya hivyo kwa sababu huku kijijini usafiri ni wa shida mno na nilitaka kumuwahi baba yangu,” alisema Bond.

Leave A Reply