The House of Favourite Newspapers

Bozi: Mastaa Tunaishi kwa kuchuna mabuzi!

img_1001      Msanii wa filamu Bongo, Fatuma Ayubu ‘Bozi’ akijiweka sawa nyumbani kwake maeneo ya Kinondoni-Studio jijini Dar

MPAKA HOME: Imelde Mtema & Mayasa Mariwata.

LEO katika kolamu hii tunaye msanii wa filamu Bongo, Fatuma Ayubu ‘Bozi’ aliyefanya poa kwenye filamu nyingi ikiwemo ya Mwanaheri. Mrembo huyu anaishi maeneo ya Kinondoni-Studio jijini Dar. Anaishi kisela kwenye chumba kimoja alichopanga.

Maisha yako yakoje?

“Kiukweli sanaa hailipi kiivyo na wala sifanyi kazi yoyote mbali na sanaa lakini maisha kwangu ni murua, kwa kuwa ni mtu wa mishemishe yaani dili lolote la hela huwa sililegezei, ndiyo maana naweza kumudu maisha yangu bila kutegemea mtu.

bozi-3Akiweka sawa vyombo vyake.

Ratiba yake ya siku ikoje?

“Nikiamka lazima kwanza nifanye mazoezi kidogo kuweka mwili sawa, kisha mambo ya usafi na madikodiko ndo yafuate, kifupi mimi si mtu wa kushinda nyumbani kwani muda mwingi nakuwa kwenye misele ya kusaka pesa, lakini huwa napenda nile chakula nilichopika mwenyewe ndiyo nitoke, kikubwa nikiwa nyumbani napenda kusikiliza muziki na kutazama muvi.

Kuchuna mabuzi je?

“Ni kweli wasanii wengi tunapenda kudanga, siwezi kuficha hata mimi ni mmoja wao katika kundi la watu wanaogawa penzi kwa mapedeshee, wengi tunafanya hivyo sababu ya maisha mazuri na kuendana na hadhi ya majina yetu kwa mashabiki, maana msanii haupaswi kuwa mchafu mchafu lazima upendeze.

Hajui kusema ‘no’ mbele ya mkwanja?

“Hiyo siyo kweli bwana, hata kama mtu ana hela kama hajanivutia siwezi kuwa naye, hata hayo madanga mpaka nivutiwe naye ndiyo napata hata mzuka wa kumlia pesa zake vinginevyo siwezi kumkubali, natoka na mtu mwenye sifa ninazozihitaji yaani awe ana mvuto uliokithiri (HB) na mkwanja ndio mpango mzima.

bozi-4Muonekano wa nyumba anayoishi maeneo ya Kinondoni-Studio jijini Dar.

Anatumia mkorogo?

“Hilo kwangu hapana hii rangi ya chungwa nimezaliwa nayo, wengi wanafanya hivyo wakiamini ni njia moja wapo ya kuongeza urembo na kuvutia zaidi lakini madhara yake ni makubwa mno, yasipotokea ujanani basi utajuta uzeeni, sithubutu kamwe.

bozi-5Bozi akiwa katika pozi.

Kuna madai kamari inakufilisi?

“Da sijui nilizungumziaje hilo jamii inielewe, bora nikaweka wazi ili nisaidiwe kuweza kuacha maana narudi nyuma kimaisha, naweza kwenda hata na laki tano nikaliwa yote bila kuambulia faida, sababu ya kucheza kamari nimekuwa kama mteja wa unga kwenye hilo, hiki chumba kilijaa lakini nimebebewa vitu vingi likiwemo kabati, Tv, deki kwa kuviweka bondi huko.

bozi-2Akifanya usafi.

Kwenye mahusiano vepe?

(Hahaha) nina mpenzi lakini sitaki kumuongelea sana kwa sasa, sababu bado namchunguza tabia maana sina muda mrefu naye kwenye mahusiano, naweza nikajiaminisha kuwa nimefika kumbe mwenzangu anapita njia kwa kutaka ujiko wa kutembea na msanii, nikimuona amekaa kwenye mstari nitamuanika.

Vipi kuhusu madanga na huyo uliyenaye?

“Hii ni siri yangu, tukifikia wakati mzuri wote nitawaacha nitabaki naye tu.”

Comments are closed.