The House of Favourite Newspapers

Bukoba: Wamachinga Wavamia Kingo za Barabara, Wapanga Bidhaa Kufuatia Agizo la JPM Jana

bgukoba-machingaBUKOBA: Baadhi ya wafanyabiashara ndogondogo katika manispa ya bukoba maarufu kwa jina la wamachinga waliokuwa wameondolewa kwenye maeneo ya kingo za barabara zilizoko katika maanispaa hiyo baada ya kutengewa eneo la machinjio ya zamani kwa ajili ya kuendesha shughuli zao za kibiashara leo wameyavamia tena maeneo ya kingo hizo za barabara na kupanga bidhaa zao kwa kisingizio cha kwamba Rais Magufuli ameagiza wasibugudhiwe.

Wamachinga hao huku wakiimba nyimbo za kumsifu Rais John Pombe Magufuli wamesema wamelazimika kuyavamia maeneo ya kingo za barabara baada ya kusikia agizo la rais la kutaka wasibugudhiwe kwa kuwa eneo la machinjio ya zamani lilitengwa na manispaa ya Bukoba kwa ajili ya kuendesha biashara ya kuwa lilikuwa sio rafiki kwao.

Mapema 6 Desemba 2016 Rais Dkt. John Magufuli alimuagiza Waziri na Katibu Mkuu Ofisi ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kusitisha mara moja mpango wa kuwaondoa wafanyabiashara wadogo (MACHINGA) jijini Mwanza na mikoa mingine nchini, huku akjizitaka mamlaka hizo kukamilisha maandalizi ya maeneo ambayo watawahamishia wafanyabiashara hao kwa kuwashirikisha wamachinga wenyewe.

Rais Magufuli akiwa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan alitoa agizo hilo jijini Dar es Salaam na kuonya kuwa kiongozi yeyote asiye tayari kutekeleza agizo hilo aachie ngazi.

Katika hatua nyingine Rais Magufuli pia aliiagiza wizara ya nishati na Madini kusitisha mara moja mpango wa kuwaondoa wachimbaji wadogo katika kijiji cha Nyaligongo kata ya Mwakitolyo mkoani Shinyanga na badala yake wachimbaji hao waachwe waendelee na shughuli zao na hivyo leseni ya mwekezaji anayedai eneo hilo ni lake aondolewe.

“Wale waliofukuzwa Shinyanga wabaki palepale, kama ni leseni ya huyo mwekezaji ifutwe, Mhe. Makamu wa Rais fuatilia hili, mweleze Waziri wa Nishati na Madini, waache kufukuza wananchi hovyohovyo, wale wanapata riziki yao, wanasomesha watoto wao lakini wanafukuzwa tu.

“Na hizi ndio ajira zenyewe, tulisema tunatengeneza ajira, wewe mwekezaji ni mmoja unakwenda kuwafukuza watu 5,000? haiwezekani na wala haingii akilini” amesisitiza Rais Magufuli.

Rais Magufuli alikemea vitendo vya wawekezaji wakubwa kupewa maeneo ambayo wachimbaji wadogo wanaendesha shughuli zao tena kwa mtindo kwa kutengeneza nyaraka zinaonesha mwekezaji husika alipewa eneo hilo kabla ya wachimbaji wadogo na kusisitiza kuwa mchezo huo hautavumiliwa.

Ilikupita hii ya Magufuli Kuwaruhusu Wamachinga Jiji la Mwanza na Wachimbaji Wado Shinyanga?

halotel-strip-1-1

Comments are closed.