The House of Favourite Newspapers

Celine Dion Afunguka Kifo cha Mume, Ujio Wake Mpya

JUMATANO Septemba 18, Celine Dion alifanya mahojiano na gazeti moja la burudani na kuzungumzia  mambo kadhaa ukiwemo ujio wa albamu yake mpya ya  ‘Courage‘ na jinsi alivyopata uvumilivu baada ya kufiwa na mume wake René Angélil  mwaka 2016.

 

Courage’  itaingia sokoni Novemba 15, mwaka huu na itakuwa albamu ya kwanza ya Celine Dion  bila kuwepo ushdiriki wa mume wake. ”Ninaposema, bila Rene namaanisha, Rene ataendelea kuwa sehemu ya maisha yangu kila siku,” alisema  Dion.

“Alikuwa ni mtu ambaye kabla sijaongea tayari aliyasoma mawazo yangu, angekuwepo sasa hivi angekuwa anafanya mengi lakini inabidi nikubaliane na ukweli kwamba sitamuona tena, hivyo natakiwa kuhakikisha natumia nafasi yangu kuendesha maisha yangu na watoto,”  aliongeza.

Kwenye albmu hiyo, amesema nyimbo nyingi zinelezea maisha baada ya kumpoteza mume wake ambaye alikuwa ni meneja wake na baba  watoto wake ambao pia wanamiss mapenzi ya baba yao.

Mwanamama huyo mwenye miaka 51 alipoulizwa kuhusu mahusiano mapya baada ya mume wake kufariki, amejibu: “Nina bahati sana kuwa na watu wanaonizunguka na kunifanya nifurahi muda mwingi”.

Kwenye kauli yake nyingine  amesema vitu anavyokumbuka kutoka kwa mume wake ni kuguswa, kukumbatiwa na kuambiwa yeye ni mrembo.

Comments are closed.