The House of Favourite Newspapers

Chama Cha Waigizaji wampongeza JPM

0

1.

Katibu wa Chama Wasanii Mkoa wa Kinondoni, Jafari  Dionizi (wa kwanza kushoto) akisoma taarifa yake.

2

Kutoka kushoto: Mjumbe wa chama, Ahmed Olotu (Mzee Chilo), Jafari Dionizi na Mwenyekiti wa chama hicho, Ali Baucha wakiwa kwenye mkutano huo.

3

Wanahabari wakichukua tukio hilo.

NA DENIS MTIMA/GPL

CHAMA  Cha Waigizaji Mkoa wa Kinondoni leo kimetoa pongezi kwa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa kazi yao nzuri tangu ishike madaraka.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, Katibu wa chama hicho, Jafari  Dionizi alisema anampongeza  rais kwa kuunda Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo na kumteua mtu shupavu, mchapakazi, jasiri katika maamuzi, Nape Nnauye ambaye ana kasi kubwa ya kugundua wizi mkubwa wa kazi za wasanii na kuwakamata wahalifu hao.

“Namuomba Waziri Nape afanye zoezi hilo kuwa endelevu kwani litafanya wasanii kunufaika na matunda ya kazi zao,” alisema.

Leave A Reply