Alt name

Championi yapendezesha ‘vibanda umiza’ Dar

1          Ofisi Masoko wa Kampuni ya Global Publishers, Yohana Mkanda (kushoto) akimkabidhi Karim Simba, mkazi wa Kinondoni Mkwajuni ubao wa kuandikia ratiba za kuonesha mpira.

2 Mkanda akimkabidhi ubao wa kuandikia ratiba za kuonesha mpira, Niga Juma, mkazi wa Magomeni Mwembe Chai.

3 Diego Kawawa (kulia), akikabidhiwa ubao.

4 Kened Lameck (kulia), mkazi wa Manzese Midizini akikabidhiwa ubao wake.

5 Abdulaziz Ahmed (kulia), mkazi wa Tabata Kimanga akikabidhiwa ubao wake.

6 Omega Himili (kulia), mkazi wa Tabata Mawenzi akikabidhiwa ubao wake.

7 Peter Maeda (kulia), mkazi wa Kimara Bonyokwa akikabidhiwa ubao wake.

8Mwaiwe Leonard (kulia), akipokea ubao wenye nembo ya Gazeti la Championi.

9 Hamis Abdallah ( kulia), mkazi wa Kimara Mwisho akikabidhiwa ubao wake.

10 Rajab Yusuph (kulia), akipokea ubao wake.

GAZETI  namba moja la michezo Tanzania la Championi, leo limegawa mbao za matangazo kwa baadhi ya sehemu za kuoneshea mpira maarufu kama vibanda umiza vilivyopo maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar.
Zoezi hilo la ugawaji wa mbao hizo limefanywa kwa nia ya kulitangaza gazeti hilo linalomilikiwa na Kampuni ya Global Publishers Ltd na kuwajali wapenzi wa soka nchini, ambapo ofisa masoko wa kampuni hiyo, Yohana Mkanda alizunguka maeneo mbalimbali yakiwemo Mkwajuni, Tabata, Kimara na Mbezi ambapo wenye vibanda walinufaika na mbao hizo.

“Lengo letu ni kuimarisha uhusiano kati yetu na mashabiki wa soka ambao ndiyo wadau wakubwa wa gazeti la Championi, tutaendelea kuzunguka sehemu nyingine nyingi kugawa mbao hizo,” alisema Mkanda.

 

Na Denis Mtima/Gpl

Leave A Comment

Related Posts