The House of Favourite Newspapers

Choki Ana Siri ya Kudorora kwa Muziki wa Dansi, Kisa cha Kuikacha Bendi Yake na Kurudi Twanga

choki-1 DAR ES SALAAM: Msanii mkongwe kwenye tasnia ya muziki wa dansi hapa Bongo, Ali Choki ‘Mzee wa Farasi’ leo ameamua kufunguka ya moyoni kuhusu kwa nini muziki huo umekuwa ukishindwa kutusua na kufika mbali kama inavyofanyika kwenye miziki mingine kama ya bongo fleva na singeli.

choki-2Ali Choki (katikati) akiwa na wahariri; Sifael Paul wa Gazeti la Ijumaa Wikienda (kushoto) na Elvan Stambuli wa Gazeti la Uwazi (kulia).

Akihojiwa kwenye kipindi cha exclusive interview cha Global TV Online, Choki aliyewahi kutamba na nyimbo zake kama majirani, regina na nyingine amesema kuwa, kisa cha kudorora kwa dansi; Kwanza ni nyimbo kuwa ndefu, dakika 10 hadi 15 kiasi ambacho unaweza kumboa msikilizaji au mtazamaji tofauti na bongo fleva ambayo wimbo unakuwa wa dakika 3 au 4 tu na unakuwa umebeba kila kitu kinachotakiwa kuwemo.

choki-3Choki akiwa na Msanifu Kurasa wa Magazeti ya Global Publishers, Charles Mgela.

Jambo jingineni ubora na ubunifu katika video za dansi, Choki amebainisha kuwa video nyingi za muziki wa dansi hazina ubunifu mzuri kivile, waimbaji wanakuwa wengi kama kwaya pamoja na wanenguaji jambo ambalo pia linaweza kumboa msikilizaji wa wimbo au mtazamaji wa video.

choki-4Choki akiwa na Mhariri wa Gazeti la Championi Ijumaa, John Joseph.

Ili kuboresha hayo, Choki ameshauri hata kama waimbaji wa muziki wa dansi watakuwa wengi lakini kwenye video aonekane mmoja au wawili tu pamoja na ma-video queen wenye mvuto na sio kujaza rundo la waimbaji na madensa hasa kwenye video. Pia video ziboreshwe, location nzuri, mavazi na kupunguza urefu wa wimbo. Ubunifu zaidi uongezwe hasa kwenye video ili kuendana na soko la muziki maana video ndiyo inamtambulisha zaidi msanii na ubora wa kazi zake.

Mbali na hayo ya kuboresha muziki wa dansi, Choki pia ameeleza sababu ya yeye kushindwa kumudu kuwa na bendi yake ya x-tra Bongo aliyoianzisha maiaka ya nyuma na badala yake kuivunja na kurudi tena kwenye bendi yake ya zamani ya Twanga Pepeta inayoongozwa na Asha Baraka.

“Kushindwa kuendesha bendi yangu (X-Tra Bongo) ni sababu za kibiashara, nilichokuwa nakitarajia sikukipata japo nilivumilia kwa miaka mitano bila mafanikio, cha zaidi labda niliongeza vyombo vyenye ubora lakini sikupata mafanikio kama nilivyotarajia wakati nafungua bendi yangu”amesema Chok.

“Mbali na hivyo hata kuna wakati nilisafiri kwenda japani na Finland kuutangaza muziki wangu nikiwa na Super Nyamwera, gharama ilikuwa kubwa sikuweza kumudu kwenda waimbaji wote jambo ambalo kumbe liliwakasilisha waliobaki, na nilivyorudi kutoka safari nikajikuta nimefanyiwa fitina, waimbaji wangu wote wameondoka hawapo kwenye bendi, iliniiuma sana nikaona hakuna ninachokifanya ni bora bendi ife tu”, alimalizia kusema Choki.

Stori na Edwin Lindege, Picha na Kelvin Shayo/GPL

Comments are closed.