The House of Favourite Newspapers

Chozi la Kanumba kwa Maya halikauki

0

WM-4Mayasa Mrisho ‘Maya’ na Kanumba enzi za uhai wake.

STORI: Imelda Mtema, Wikienda

Dar es Salaam: Mwigizaji wa kitambo Bongo, Mayasa Mrisho ‘Maya’ amefunguka kuwa chozi lake kwa aliyekuwa mwigizaji mwenzake aliyemfanya kaka yake wa hiari, marehemu Steven Kanumba halikauka siku zote pamoja na kwamba ni takriban miaka minne tangu alipoaga dunia Aprili 7, 2012.

BIRTHDAYKANUMBA3Maya akiliakwa uchungu

Akizungumza na Wikienda, Maya alisema kuwa, mara nyingi watu huwa hawamuelewi lakini ukweli ni kwamba thamani ya uigizaji wake imepotea tangu alipoondoka Kanumba kwani ndiye aliyekuwa akimtia moyo.

KanumbaMarehemu Kanumba

“Tunaweza kuwa lokesheni, nikajikuta nikidondosha machozi na hapo watu watafanya kazi sana kuniweka sawa ili niweze kuendelea. Ni kama maisha yangu kwani mara nyingi najikuta nalia sana kwa ajili ya Kanumba,” alisema Maya aliyekuwa mtu wa karibu wa staa huyo.

Leave A Reply