The House of Favourite Newspapers

Cristiano Ronaldo Anyakuwa Tuzo ya Mwanasoka Bora Ulaya

0

UEFA (1)Mshambuliaji wa Klabu ya Real Madrid na Timu ya Taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo jana alitangazwa kuwa mwanasoka Bora Ulaya baada ya kushinda tuzo hiyo kwa mara ya tatu sasa.

UEFA (2)Ronaldo alitangazwa kuwa Mwanasoka Bora wa Ulaya baada ya kuwashinda wachezaji wenzke ambao ni Gareth Bale wa Real Madrid na Timu ya Taifa ya Wales pamoja na Antonio Greizman wa Athletico Madrid na Timu ya taifa ya Ufaransa ambapo klabu zao wote ni za Jiji la Madrid nchini Hispania.

UEFA (3)

KURA

Katika Kura zilizopigwa na waandishi 55 wanachama wa UEFA katika Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ulaya 2015/2016 matokeo yalikuwa.

Cristiano Ronaldo – 40

Antoine Griezmann – 8

Gareth Bale – 7

UEFA (4)

Ronaldo mwenye umri wa miaka 31, ameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ulaya mara tatu sasa huku. mara ya kwanza alishinda tuzo hiyo mwaka 2008 akiwa na Manchester United, pia akiwa na Real mwaka 2014.

UEFA (5)Griezmann akiselfika na mashabiki wake jana wakati wa tuzo hizo

CquGSTEWIAACxnYMshambuliaji wa Olympique Lyon na timu ya Norway Ada Hegerber ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Ulaya kwa upande wa Wanawake 2015/2016

UEFA (6)

Bale alizungumzazjana wakati akihojiwa na WalesOnline: ‘Nilikuwa na bahati kushinda European Super Cup huko Cardiff na ilikuwa jambo la kushangaza kwangu, kwa familia yangu na marafiki pia.

‘Lakini Champions League ni levo nyingine kabisa. ni maalum kwa ajili ya Real Madrid tutaendelea kushinda tena na tena na kuwek historia kubwa juu ya hili.’

UEFA (7)

Baada ya kushinda tuzo hiyo jana, Ronaldo alisema: ‘Ni jambo la kushukuu. Wachezaji wenzangu wamekuwa nguzo kubwa ya mafanikio yetu kila mwaka. Ninafanya kazi kwa bidii na kujituma lakini bila wao isingewezekana.

UEFA (11)‘Asanteni wachezaji wenzangu wa Real Madrid na ureno. [Washindi wa Euro 2016] nimeshinda mataji matatu ya Champions League mwaka huu. Kushinda nikiwa na Timu ya taifa ni jambo la heri sana.’ Alisema Ronaldo

UEFA (8) UEFA (9) UEFA (10)  UEFA (12)

Leave A Reply