Diamond, Shetta ‘Wapeana fangasi’ kiaina
Stori: Hamida Hassan
Diamond
Juzikati ilitupiwa picha mtandaoni ikimuonesha Diamond akiwa amevaa sandozi f’lani zenye rangi nyeusi na nyeupe, watu kibao waka-like, baadaye viatu hivyo vikaonekana vimevaliwa na Shetta na hapo ndipo gumzo likaanza.
Wengi walihoji mtu halali anayevimiliki, huku baadhi wakidai eti Shetta ndiye aliyeomba deiwaka ili apigie picha.
Shetta
Mbali na yote, mchangiaji mmoja mwenye jina la Wizmafet kwenye mtandao wa Instagram akachambua madhara ya watu kuvaliana viatu na kueleza kuwa, kwa kufanya hivyo kuna uwezekano wa kuambukizana fangasi.