The House of Favourite Newspapers

Diwani Aibuka Kinara Riadha

0

1 (1) 1 (2)

Diwani wa Viti Maalum Kata ya Matalawe Manispaa ya Songea, Judith Mbogoro akimalizia mbio za kilometa 5, katika Tamasha la Majimaji Selebuka linaloendelea kwenye Uwanja wa Makumbusho ya Mashujaa wa Vita ya Majimaji mjinini Songea. Tamasha hilo limekata utepe Mei 28 na litafungwa Juni 4, mwaka huu.2 (1) 2 (2)Bingwa wa mbio fupi za Km 5 kwa wanawake, Judith Mbogoro akiwa na washindi wa mbio hizo kwa upande wa wanaume. Kutoka kulia ni kinara Hamad Rashid na mshindi wa pili, Ferdinand Haule.

3Bingwa wa mbio ndefu Km 21, John Mahangula akikata upepo kuwania zawadi ya mshindi wa kwanza katika tamasha la kila mwaka la Majimajia Selebuka linaloendelea mjini Songea katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Mashujaa wa Vita vya Majimaji.4 (1) 4 (2)Washiriki wa mbio fupi za Km 5 wakichuana kuwania zawadi kwa washindi wa kwanza hadi watatu.

5 (1) 5 (2)Theresia Tembo akishangilia baada ya kushika nafasi ya tatu kwenye mbio za Km 5 kwa upande wa wanawake.7

Mratibu wa tamasha, Reinafrida Rwezaura naye alishiriki mbio fupi Km 5 akipokea cheti kutoka kwa Diwani wa Kata ya Songea Mjini, Shaibu Kitete. Kushoto kwake ni Diwani wa Kata ya Matalawe, Judith Mbogoro na balozi wa tamasha kwa upande wa Marekani, Anna Schwartz.

 

IMG_9175 IMG_9196

KAMA kawaida yake! Ikiwa ni siku ya kwanza tangu kufunguliwa kwa tamasha pendwa la Majimaji Selebuka tayari vituko, mbwembwe kutoka kwa viongozi wa kiserikali vimeanza kujitokeza hii ni baada ya Diwani wa Kata ya Matalawe Manispaa ya Songea, Judith Mbogoro kuibuka kinara wa mbio za Km 5 kwa upande wa wanawake.

Tamasha hilo limekata utepe leo Mei 28 na litafika tamati Juni 4, mwaka huu na linaganyika kwenye Uwanja wa Makumbusho ya Mashujaa wa Vita vya Majimaji mjini Songea, Ruvuma

Judith alitumia muda wa dakika 27:28, akifuatiwa na Fatuma  Ching’ang’a aliyetumia dakika 28:46 huku Theresia Tembo akimaliza wa tatu akihitimisha kwa muda wa dakika 30:26.

Akizungumzia ushindi wake, Judith alisema siri ya ushindi kuwa ni mazoezi kila siku, kupumzika muda mrefu na mlo mzuri.

“Tofauti na Jumapili kila siku nafanya mazoezi nazunguka uwanja wa mara tano, sinywi pombe, nalala muda wa kutosha (masaa 8) na kula vizuri (diet) ndiyo maana nimeweza achilia mbali umri wangu kunitupa mkono (miaka 38),” alisema Judith.

Kwa upande wa wanaume, kinara alikuwa Hamad Rashid aliyetumia dakika 16:59, nafasi ya pili Ferdinand Haule aliyetumia dakika 18:22 wakati nafasi ya tatu ilichukuliwa na Nathan Mpangala aliyetumia dakika 29:19 ambaye mbali na ushiriki huo, pia ni balozi wa tamasha.

Katika mbio za Km 21, John Mahagula aliibuka kinara kwa kutumia muda wa saa 1:32: 14, Jackson Faustine nafasi ya pili saa 1:41:17 na nafasi ya tatu ilichukuliwa na  Abdallah Oscar aliyetumia muda wa saa 1: 50:48.

Washindi wote wameondoka na vitita vya fedha taslim, medali na vyeti vilitolewa kwa washiriki wote.

Kesho Jumapili ni mashindano ya Ngoma za Asili, maonyesho ya ujasiriamali pamoja na utalii wa ndani katika vivutio vya mbuga za wanyama.

 PICHA NA NICODEMUS JONAS, GPL

Leave A Reply