The House of Favourite Newspapers

Drake Amtambulisha Taylor Swift kwa Mama Yake, Penzi lake na Rihanna Njia Panda

 omg-what-if-taylor-swift-and-drake-date__opt

RAPA Aubrey Drake Graham, ‘Drake’ amempa hadhi ya juu mwanadada Taylor Swift ikiwemo kumtambulisha kwa mama yake pamoja na watu wake wa karibu zikiwa ni ishara za awali za kuonyesha mahusiano yao.

Tukio hilo lilitokea Jumapili iliyopita wakati wa sherehe ya Drake kutimiza umri wa miaka 30 iliyofanyika Los Angeles nchini Marekani.

1026-drake-taylor-swift-2013-vma-getty-3

Drake na Taylor mwaka 2013.

Kitendo hicho kimemake headlines katika mitandao ya kijamii kikiashiria Drake na Taylor kuwa na mahusiano huku kikiongezwa uzito na mwanadada Rihanna ambaye hakuhudhuria sherehe hizo.

rs_1024x759-160828205712-1024-drake-rihanna-mtv-vmas-performance-5

Drake na Rihanna.

Kwa mujibu wa chanzo kilichokaribu na Rihanna ambaye ndiye mpenzi wa Drake, ni kwamba alihuzunika baada ya Taylor kuonekana kuchukua nafasi yake kwa kuwa gumzo katika sherehe hiyo na kuwa staa huyo anajilaumu kwa nini hakuudhuria sherehe.

NEW YORK - DECEMBER 08:  *Exclusive Coverage*  Musician Taylor Swift and singer Rihanna attend  the launch of VEVO, the world's premiere destination for premium music video and entertainmentat Skylight Studio on December 8, 2009 in New York City.  (Photo by Theo Wargo/Getty Images for VEVO)

Rihanna na Taylor mwaka 2009.

Comments are closed.