Ebitoke Agoma Kutoa Mimba ya Mlela

BAADA ya kuibua tumbwili hotelini kwa aliyedai ni mpenzi wake, mwigizaji Yusuf Mlela, mchekeshaji Annastasia Exavery ‘Ebitoke’ amesema, mimba aliyonasa ya jamaa huyo hawezi kuitoa hata kama atashikiwa mtutu wa bunduki.

 

Kufuatia kusambaa kwa ubuyu huo kuwa Ebitoke ni mjamzito, Gazeti la Ijumaa Wikienda lilimtafuta ili kuthibitisha kama kweli ana mimba au ni stori za mitandaoni tu.

Ebitoke ameliambia gazeti hili, hawezi kujisingizia jambo kama hilo na kuongeza kuwa, pamoja na kwamba ametibuana na Mlela, lakini hawezi kuutoa ujauzito huo.

 

Amesema kilichomfanya akapata hasira na kwenda kumfanyia fujo Mlela ni kwa sababu jamaa huyo aliahidi kuhudumia mimba yake hiyo, lakini ghafla akashtuka anamsaliti na kwenda kwa Stella au Beyonce.

 

“Kwanza ninamshukuru Mungu kwa kunijaalia nami nimepata ujauzito kwa sababu wengi wanaomba wapate mimba bila mafanikio.

 

“Nimesema piga, ua, siwezi kutoa hii mimba kwa sababu ya ujinga wa mtu. Nikizaa atahudumia mtoto kwani ananijua vilivyo, nitaenda kumuanzishia tena,” alisema Ebitoke.


Loading...

Toa comment