The House of Favourite Newspapers

Ebitoke: Muvi ya Mapenzi Yangu na Mlela Inakuja

Mwanadada Ebitoke akiwa na Yusuph Mlela.

MKALI wa vichekesho kwa lafudhi ya Kihaya, mwanadada Ebitoke, amesema kuwa wanaandaa muvi itakayoonyesha mahusiano yake na mpenzi wake wa sasa ambaye pia ni muigizaji wa Bongo, Yusuph Mlela.

 

Ebitoke aliyasema hayo alipotembelea Ofisi za Global Group zilizopo Sinza Mori hivi karibuni na kufanya mahojiano katika Kipindi cha Mid Morning Fresh kinachorushwa na +255 Global Radio, ambapo alikiri kuwa katika mapenzi mazito na Mlela na huenda akamzalia mtoto.  

Akizungumzia muvi hiyo, Ebitoke alisema; “Unajua mimi na Mlela tumekuja na wazo la kuandaa kitu kama muvi ambayo itakuwa na matukio ya ukweli kuhusu mahusiano yetu, yaani yataonyesha tangu tulivyokutana Zanzibar, tulivyoanza kupendana na hadi hapa tulipofikia na pengine kuendelea huko mbele.

“Mimi na Mlela ni zaidi ya wapenzi, kwa sababu ule upendo umepitiliza kiasi kwamba nashindwa kueleza kwa maneno, hivyo wale ambao wanatamani kujua mapenzi yetu yalipoanzia wakae tayari, kwa kuwa muda wowote muvi itakuwa tayari.”

 

Unaweza kuisikiliza +255 Global Radio kwa kupakua App ya 255Global Radio pale play store na unaweza kusikiliza online saa 24, kupitia tovuti ya www. globalradio.co.tz

Comments are closed.