The House of Favourite Newspapers

Efm Wawachapa Bongo Fleva

0

1. Kikosi cha timu ya Bongo Fleva kikionekana kiko maridadi kabisa.

Kikosi cha timu ya Bongo Fleva.

2.Timu ya Wafanyakazi wa kituo cha redio cha Efm kama wanavyoonekana.

Timu ya wafanyakazi wa kituo cha redio cha Efm.

WAFANYAKAZI wa kituo cha redio cha Efm kilichopo Kawe jijini Dar es Salaam, jana waliichapa timu ya Bongo Fleva mabao 4 kwa 3 katika mchezo wao uliofanyika katika viwanja vya Tanganyika Packers, jijini Dar.

Katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo, msanii Khalid Mohammed (TID) alifunga bao la kwanza, la pili likifungwa na H. Baba kwa mkwaju wa penati na la tatu likifungwa na Ali Kiba.
Kwa hatua nyingine, wafanyakazi wa Efm wakiongozwa na kapteni Dennis Ssebo waliweza kuwachapa mabao manne wapinzani hao.

Akiongelea mchezo huo,  Ssebo alisema lengo la mchezo huo lilikuwa ni kuwaweka karibu wasanii na kituo chao na kuimarisha afya zao.

3.Baadhi ya mashabiki waliojitokeza kufuatilia mchezo .

Baadhi ya mashabiki waliojitokeza kufuatilia mchezo huo.

7. TID akijalibu kumtioka mchezaji wa Efm

TID akijaribu kumtoka mchezaji wa Efm.

6. Kiungo mkabaji wa timu ya Bongo Fleva Stamina akionekana kwa umaridadi kabisa.

Kiungo mkabaji wa timu ya Bongo Fleva, Stamina.

5. Wahezaji wote wa timu mbili wakipeana mikono kwa ishala ya kuimarisha upendo.5............

Wachezaji wote wa timu mbili wakipeana mikono kama ishara ya kuimarisha upendo.

4. Timu zikitifuana vilivyo.

Timu zikitifuana vilivyo.

8. Khalid Mohamed ( T I D) Akishangilia goli lake la kwanza baada ya kutupia kambani dakika ya 35 ya kipindi cha kwanza na ndio alionekana kuwa nyota wa mchezo huo.

Khalid Mohamed (TID) akishangilia goli lake la kwanza baada ya kutupia kambani dakika ya 35 ya kipindi cha kwanza na ndiye aliyekuwa nyota wa mchezo huo.

9. Young Kira pamoja na Huseni Machozi wakitoka uwanjani kwenda kupumzika baada ya kipindi cha kwanza kumalizika.
Young Killer na Hussein Machozi wakitoka uwanjani wakati wa mapumziko.

10. Mzunguko wa kipindi cha pili ukiendelea vikali

Mzunguko wa kipindi cha pili ukiendelea.

Na Hilaly Daud/GPL

Leave A Reply