The House of Favourite Newspapers

EFM Yamfikisha Kortini Paul James, Yamdai Fidia ya Tsh. Milioni 200

picha-ya-pj-530x3532xDAR ES SALAAM: Mtangazaji mahili wa Kituo cha Redio cha Clouds FM, Paul James ‘PJ’ amefikishwa katika Mahakama ya Kazi yaa jijini Dar es Salaam na Kituo cha Redio cha EFM kwa madai ya kuvunja mkataba kinyemela.

efm-radio-page-001PJ aliondoka EFM mwanzoni mwa mwezi Oktoba na kurejea Clouds FM alikokuwa akifanya kazi kabla ya kuondoka pamoja na mtangazaji mwenzake Gerald Hando.

EFM imefungua mashtaka katika Mahakama ya Kazi jijini Dar es Salaam kwa madai ya kukiuka mkataba wa kazi na kituo hicho.

Kufuatia mashtaka hayo, EFM inadai fidia ya pesa kiasi cha Tsh. Milioni 200 kutoka kwa mtangazaji huyo.

Inadai PJ alikatisha mkataba kiholela na kurudi tena Clouds FM bila kufuata makubaliano pamoja na sheria alizokubaliana nazo katika mkataba wake pale alipojiunga nacho.

Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa November 23, 2016 katika Mahakama ya Kazi ya jijini Dar es Salaam.

Comments are closed.