The House of Favourite Newspapers

Esha Buheti ageukia pombe

0

EsheBuhetiIMELDA MTEMA, Amani

MKALI wa filamu za Kibongo, Esha Buheti ameweka wazi kwamba hivi sasa ameamua kugeukia pombe kutokana na msongo wa mawazo alionao.

Esha aliliambia Amani kuwa, awali alikuwa hapendi kuju-muika na watu wanaokunywa pombe lakini kutokana na vitu ambavyo vinamtokea mwanadamu katika maisha (stress) naye amejikuta akijiingiza huko kitu ambacho hakukipanga.

“Pombe ilikuwa sumu kabisa katika maisha yangu lakini kutokana na stress ambazo siwezi kuziweka wazi zimenifanya niizoee kunywa,” alisema Esha.

Hii si mara ya kwanza Esha kukataa kitu na kuja kukifanya. Kipindi cha nyuma aliwahi kujiapiza kuwa hatakuja kujichora ‘Tattoo’ mwilini mwake mpaka anaingia kaburini lakini alikuja kwenda kinyume na maneno yake na kuji

chora.

Leave A Reply