The House of Favourite Newspapers

Faiza, Wema ndani ya bifu nzito

0

Faiza AllyFaiza Ali.

IMELDA MTEMA, IJUMAA

MTIFUANO wa maneno makali umeibuka kati ya wasanii wa fi lamu Bongo, Wema Sepetu na Faiza Ali chanzo kikiwa ni Faiza kuposti maneno ya ‘kumdis’ Wema kutokana na mfumo wake wa maisha ya kimapenzi.

wemaa-1Wema na Idris.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Faiza aliandika kuwa Wema anapenda sana ‘ving’asti’ (dogodogo) akitolea mfano Idris Sultan aliyekuwa mpenzi wake, kisha akasema kuwa anaomba Mungu asije akapata mtoto wa kiume atakayependa ku-date na wanawake waliomzidi umri.

Kutokana na maneno hayo yaliyojaa shari ndani yake, Ijumaa lilimtafuta Wema kuzungumzia posti hiyo ambapo alipopatikana alikuwa na haya ya kusema: “Yaani mimi simpendi kabisa yule binti, namuona ni mpumba** tu, ndiyo maana hata Sugu akaona si mwanamke anayefaa kuwa mkewe. Hana akili kabisa.”

Leave A Reply