The House of Favourite Newspapers

Fellaini Aiingiza Mkenge Man United, Mourinho Ajikosha

1crbnaikbp7fi1rycq7s5s5dgp Leighton Baines aliifungia kwa mkwaju wa penalti klabu yake ya Everton na kuiwezehsa kupata sare ya 1-1 dhidi ya Manchester United katika uwanja wa Goodison Park, jana Jumapili jioni.

Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho alitetea uamuzi wake kumwingiza Marouane Fellaini baada ya Mbelgiji huyo kusababisha penalti dhidi ya Everton na kuigharimu timu yake alama mbili.

“Everton hawachezi soka zuri tena. Wanacheza hovyo. Mfumo wao ni wa ajabu. Williams anacheza vibaya. Kila kitu ni hovyo na, wanapoteza, wanazidi kuharibika. Unapokuwa na mchezaji ambaye ana urefu wa mita mbili [mrefu], unamuingiza kushughulika nao,” Alisema Mourinho.

Mashetani Wekundu walikuwa wakiongoza tangu Zlatan Ibrahimovic alipofunga goli dakika ya 42, lakini mchezaji wa zamani wa Toffee Marouane Fellaini akitokea benchi aliwatunukia wapinzani wao tuta.

fiihkw2h1uzl1woworhwpttj8United, ambao hata hivyo walistahili kupunguzwa kuwa 10 mapema katika mechi hiyo, hadi sasa wameshinda mechi moja tu kati ya nane za mwisho Ligi Kuu na wapo pointi tisa nyuma ya vinara wa nne bora.

Pointi ya kuzungumziwa sana kipindi cha kwanza ni tukio la dakika ya 16, baada ya Marcos Rojo kumfanyia faulo Idrissa Gueye lakini akapona adhabu kali kwa kupewa kadi ya njano tu.

Paul Pogba na Ramiro Funes Mori walijaribu bahati yao kutoka umbali wa zaidi ya yadi 30, lakini hakuna aliyeweza kumsumbua kipa wa upinzani.

Licha ya kupungukiwa mbinu za ushambulizi, kwa kiasi kikubwa kutokana na uchezaji wa kujihami, Everton walifanya jitihada kutumia upande wa kushoto wa United na hapo ndipo walipoona mlango wa kujipatia pointi moja.

Meneja wa Everton Ronald Koeman amedai kuwa timu yake ilistahili kupata pointi Jumapili dhidi ya Manchester United.

Koeman aliiambia BBC Sport baada ya mechi: “Kiwango cha timu nzima kilikuwa chanya na tumeonyesha ushirikiano mkubwa tangu dakika ya kwanza. Tuliwapa United wakati mgumu kufanya chochote.

“Tuliruhusu kufungwa 1-0 kwa kosa ambalo linasononesha, kwa kweli. Pointi moja ndicho kiwango cha chini tulichostahili.

“Yalikuwa matokeo ya haki, hatujapoteza mchezo nyumbani kwa hiyo tuna furahia matokeo haya.”

Comments are closed.