The House of Favourite Newspapers

‘Fisi’ aliyefanya ngono na watoto, wajane akamatwa… kumbe ana Ukimwi!

1

MALAWI (1) Raia mmoja wa Malawi alionekana katika habari moja ya BBC akihusishwa na tambiko la usafishaji wa wasichana wadogo kupitia kushiriki ngono nao amekamatwa.

MALAWI (3)Eric Aniva amekamatwa kufuatia agizo la Rais Peter Mutharika kulingana na mkurugenzi wa mawasiliano katika ikulu ya rais Bright Molande aliyezungumza na BBC.

MALAWI (2)Amesema kuwa Bw. Aniva aliyepewa jina la utani kuwa ‘fisi’ kwa jukumu lake katika uovu huo atashtakiwa kwa kukiuka haki za watoto.

Pia amesema kuwa rais amechukizwa na yaliofichuliwa katika habari hiyo na ameapa kukabiliana na tamaduni hiyo.

MALAWI (1)Mtu aliyetajwa katika habari hiyo ambaye alifanya mapenzi na zaidi ya wasichana 104 pia imebainika kuwa alikuwa na virusi vya ugonjwa wa ukimwi.

Tamaduni hiyo ya usafishaji ilipendekezwa na kufadhiliwa na baadhi ya jamii kusini mwa Malawi lakini serikali imejaribu kuisitisha.

1 Comment
  1. kimaro says

    Hii inatisha na je serikal ya malawi itachukua hatua gani kuhusu huyo FISI na je vp km hajawambukiza wajane na wasichana wadogo

Leave A Reply