The House of Favourite Newspapers

Hatua za Kumchagua Rais wa Marekani

0

usa-flag

Na Leonard Msigwa.

Mchakato wa kumchagua rais wa Marekani na magavana hufanyika kwa wakati mmoja, na uchaguzi huu haufanywi kwa siku moja bali kila jimbo la uchaguzi nchini Marekani hupanga tarehe yake ya uchaguzi.

 

Uchaguzi huu hufanyika kwenye vituo kulingana na makazi yao. Mchakato huu umepewa jina la Early Voting.

 

Tofauti na nchi nyingine duniani kura zikishapigwa hazihesabiwi kula moja moja, kuna kitu kinaitwa State Points ambazo mgombea anazipata kwenye jimbo.

 

Wakati kura zinahesabiwa yule anayeonesha kushinda katika kura hizo hata kabla mchakato haujamalizika wanafanya kukadiria “estimation” hapa wanaangalia idadi ya watu ambao wamepiga kura kwa siku husika kisha wanaweka kwenye asilimia kwamba kashinda kwa asilimia ngapi.

 

Suala la kuhesabu kura ni kwamba, wanachukua jumla ya kura zilizopigwa, jumla ya kura za kila mgombea na jumla ya wapiga kura wote jimboni kisha wanapiga  hesabu za makadirio.

 

Hapa ndipo watu hutangaziwa kwamba mgombea fulani kashinda jimbo fulani na huwa haimaanishi kuwa kura zote zimehesabiwa bali wamefanya makadirio. Kura za ushindi kwenye jimbo ndiyo muhimu zaidi kwani atakayeshinda majimbo mengi ndiye atatangazwa kama rais.

 

Baada ya mchakato huu kumalizika tarehe 4 Novemba mwaka huu ndiyo siku rasmi ya uchaguzi nchini Marekani na watakaopiga kura siku hiyo ni wale tu ambao hawakushiriki kupiga kura kwenye majimbo kutokana na sababu mbalimbali.

 

Mpiga kura wa Marekani lazima awe mzaliwa, au aliyepata uraia kwa njia nyingine kama vile kuoa au kuolewa na raia wa nchi hiyo au yule ambaye amezaliwa nje ya nchi hiyo lakini wazazi wake ni raia wa Marekani na wakimbizi ambao wametambuliwa rasmi kama raia wa Marekani.

 

 

Leave A Reply