The House of Favourite Newspapers

Hawa Ndiyo Washindi wa Tuzo za La Liga Msimu wa 2015/16

la-ligaTuzo za La Liga Award 2015/2016 zilitolewa rasmi usiku wa Oktoba 24, 2016, tuzo za wachezaji na makocha waliofanya vizuri katika msimu wa 2015/2016 ndio zilitolewa huku Luis Suarez wa FC Barcelona akiwa mchezaji wa kwanza kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa dunia, tuzo ambayo imetolewa kwa mara ya kwanza.

Orodha ya washindi wa tuzo za La Liga msimu wa 2015/2016

Kocha wa Atletico Madrid Diego Simeone ametangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya kocha bora wa La Liga.

Luka Modric wa Real Madrid amepata Tuzo ya Kiungo Bora wa La Liga.

Marco Asensio wa Real Madrid ambaye aliyekuwa kwa mkopo Espanyol ameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora Anayechipukia.

Golikipa wa Atletico Madrid Jan Oblak ameshinda Tuzo ya Golikipa Bora La Liga.

Diego Godin wa Atletico Madrid ameshinda Tuzo ya Beki Bora.

Antoine Griezmann wa Atletico Madrid ameshinda Mchezaji Bora wa La Liga.

Luis Suarez wa FC Barcelona ameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa Dunia wa LaLiga.

Lionel Messi wa FC Barcelona ameshinda tuzo ya mshambuliaji bora wa LaLiga.

Comments are closed.