Heche Apigwa Chingi Chadema, Matiko Apeta

MBUNGE wa Tarime mjini, Ester Matiko ameshinda kiti cha Uenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Serengeti kwa kupata kura 44 na kumshinda Mbunge wa Tarime Vijijini John Heche aliyepata kura 38.

 

Akitangaza matokeo hayo jana Jumapili, msimamizi wa uchaguzi huo, Boniface Jacob ambaye pia ni Meya wa Manispaa ya Ubungo jijini Dar es salaam alisema wajumbe 85 walipiga kura.

 

Katika uchaguzi huo, Gimbi Masaba alichaguliwa kwa kura 45 kuwa makamu Mwenyekiti huku Maendeleo Makoye akishinda uweka hazina kwa kupata kura 42.


Loading...

Toa comment