The House of Favourite Newspapers

Hushiki Mimba? Soma Hapa

0

ovariancystdiagram.jpgTATIZO la kutokushika mimba ni kubwa katika jamii kuliko vile ambavyo mtu anaweza kufikiria. Na wanawake wengi wana tatizo hili, lakini hawafahamu sababu hasa zinazosababisha, huku baadhi yao, wakihusisha jambo hilo na ushirikina.

Moja ya sababu ya kutoshika ujauzito, ni ugonjwa wa Sisti au Nziba unaopatikana kwenye Ovari za uzazi (Ovarian Cyst).

Ili kuweza kuuelewa vyema ugonjwa huu, inatubidi kuelewa maana ya Ovari. Akina mama wana kitu kinaitwa tezi za uzazi zilizo katika pango la uzazi, zikiwa pacha.

Kwa hiyo, kazi kubwa ya Ovari ni kutengeneza mayai ya mwanamke (Ova) na homoni za kike ziitwazo Istrojeni (Estrogen) na Projesteroni (Progesterone). Kwa kawaida, Ovari ndicho chanzo kikubwa cha homoni za kike zinazoongoza ukuaji wa sifa za msichana kama matiti, umbo la mwili na nywele za mwilini.

Aidha, homoni hufanya kazi ya kurekebisha mzunguko wa hedhi na mimba. Sasa basi, uvimbe kwenye tezi za uzazi za mwanamke (Ovari), hutokana na mkusanyiko wa majimaji au ute mzito unaozungukwa na kuta nyembamba ndani ya tezi za uzazi.

Uvimbe huu ndiyo unaojulikana kitaalam kama Sisti kwenye Ovari hiyo. Uvimbe huu hutokea kwa wanawake wa umri wowote na mara nyingi huonekana kwa waliofikia kikomo cha umri wa kupata ujauzito.

Tezi za uzazi za mwanamke ni nini? Kwa kawaida, mwanamke anakuwa na tezi mbili katika mwili wake. Tezi moja upande wa kulia na tezi nyingine upande wa kushoto. Tezi hizi, hupatikana pembezoni mwa mfuko wa uzazi (Uterasi).

Watafiti wa mambo ya uzazi, wanasema tezi za uzazi za mwanamke huanza kuza lisha mayai ya uzazi yanayo julikana kitaalam kama Ova na mayai hayo ya uzazi hukua ndani ya tezi za uzazi ya mwanamke (Ovari) kwa kuchochewa na baadhi ya homoni, katikati ya mwezi, kwa maana ya siku ya 14, na huweza kudumu kwa muda wa kati ya saa 24-36.

Baada ya kiwango cha kichocheo/homoni ya ulutenishaji (Luteinizing Hormone) kuwa juu, mayai ya uzazi hutolewa katika kila Ovari. Kitendo hiki hujulikana kama Uovuleshaji (Ovulation) au kufikia kilele cha upevukaji wa mayai. Mayai haya ya uzazi huishi kwa saa chache mno, wa hadi saa 24, ikiwa hayatarutubishwa na mbegu (Sperms) kutoka kwa mwanaume.

Yai hili husafiri hadi kwenye mfuko wa uzazi ambako hukua na kuwa mtoto. Kama upachikwaji wa yai lililorutubishwa hautafanyika, basi ndani ya wiki mbili, Kopasi Luteamu (Corpus Luteum) huanza kusinyaa na kupotea na kusababisha kushuka kwa kiwango cha homoni aina ya Projesteroni (Progesterone) na Istrojeni (Estrogen).

Kushuka kwa viwango vya vichocheo hivi ndiyo husababisha mfuko wa uzazi kuanza kutoa mabaki ya kuta zake pamoja na yai la uzazi na hii ndiyo pale mwanamke anapotoka damu ukeni inayojulikana kama Hedhi (Menstrual Cycle).

Aina za Sisti/Nziba kwenye Ovari

 Kwa mujibu wa watafiti wa masuala ya kiafya na kisayansi, kuna aina nyingi za uvimbe kwenye tezi za uzazi za mwanamke. Hata hivyo, aina saba zifuatazo ndizo huonekana zaidi kwa wanawake wengi.

ITAENDELEA TOLEO LIJALO

KUNUNUA NA KUSOMA MAGAZETI YA GLOBAL PUBLISHERS ONLINE, INGIA HAPA==>VODACOM M-PAPER APP

*********

JIUNGE NA SOCIAL MEDIA ZETU

KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA

INSTAGRAM: @Globalpublishers

ERIC SHIGONGO INSTAGRAM: @ericshigongo

TWITTER: @GlobalHabari

FACEBOOK: @GlobalPublishers

SUBSCRIBE YOU TUBE: Global TV Online

GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE:@shigongotz

Leave A Reply