The House of Favourite Newspapers

Izzo: Biashara imenifanya nianzishe kundi

0

izzo biznez (1)MKALI wa michano kutoka Bongo, Emmanuel Simwinga ‘Izzo Bizness’ amefunguka kuwa ameamua kuanzisha kundi la muziki liitwalo The Amaizing kutokana na sababu za kibiashara.

Akichonga na Uwazi Showbiz, Izzo alisema kuwa kundi lake ni la watu wawili tu, yaani yeye na mwanadada mwingie aitwaye Abela Music na kwa sasa tayari wamefanya ngoma wanayotarajia kuitambulisha hivi karibuni kwenye media.

“Kwa muda mrefu sana nimefanya kazi bila kuwa ndani ya kundi, lakini kwa sasa nimeamua kuanzisha ili kutanua zaidi fun base yangu na kuongeza ladha ya tofauti kwenye muziki ninaoufanya, mbali na hivyo ni biashara.

“Unajua mnapokuwa mnafanya kazi watu wawili au zaidi mnaoelewana kunakuwa na hatua za haraka mnazo weza kupiga kuliko msanii akiwa peke yake,” alisema Izzo Bizness.

Leave A Reply