The House of Favourite Newspapers

Jay Z Kupiga Shoo Kwenye Tamasha la Hillary Clinton

jay-z-tidalRapa maarufu na mmliki wa Kampuni ya Muziki ya Tidal, Jay Z ‘Jigga’ anatarajiwa kupiga shoo na kumsapoti Hillary Clinton kwenye harakati zake za kuwania urais wa Marekani kupitia Chama cha Democratic.

Jay Z amekubali kutumbuiza kwenye tamasha kubwa na aina yake la mgombea huyo wa urais kupitia Chama cha Democratic huko Cleveland kabla ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo, shoo ambayo haijaelezewa itafanyika lini, licha ya mtandao wa Cleveland.com, kuthibitisha kuwa Jigga atatumbuiza na kuongeza kuwa, shoo hiyo itatumika kushawishi zaidi wapiga kura wamchague Clinton.

WASHINGTON, DC - APRIL 22:  Democratic presidential candidate and former U.S. Secretary of State Hillary Clinton delivers remarks at the Hillary Rodham Clinton Awards for Advancing Women in Peace and Security at Georgetown University April 22, 2015 in Washington, DC. The awards were given to former United Nations Envoy for Afghanistan Staffan de Mistura, and Dr. Miriam Coronel-Ferrer, who served as the Chief Negotiator of the Philippines Government in the Mindanao Peace Talks.  (Photo by Win McNamee/Getty Images)

Hillary Clinton

Miaka minne iliyopita, Jay Z aliungana na Bruce Springsteen kutumbuiza kwenye tamasha la Rais Barack Obama, siku moja kabla ya uchaguzi.

jay-z-hillary-clinton 

Clinton amekuwa kwenye mchuano mkali Donald Trump wa Republican huku wote wawili wakiwa kwenye upinzani mkali kati yao.

Trump amekuwa akipondwa na rappers, wakiwemo YG, Nipsey Hussle, Macklemore, Rick Ross, na G-Eazy, Clinton amekuwa akisapotiwa na wsanii kibao maarufu kama Pusha T, Common, Chance the Rapper, na will.i.am.

 

Comments are closed.