The House of Favourite Newspapers

Jeshi la Polisi: Kesi 23 za Ufisadi Zipo kwa DPP

0

1.Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Kamishna Diwan Athuman akisoma taarifa yake.-001Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Kamishna Diwani Athumani, akisoma taarifa.
2.Mkurugenzi wa mashtaka DPP, Biswalo,E.Mganga ( katikati) akitoa ufafanuzi kwa wanahabari baada ya kupokea maswali yaliyokuwa yakiulizwa.-001Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Biswalo Mganga (katikati) akitoa ufafanuzi kwa wanahabari waliouliza maswali.
3.Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya JInai,Kamishna Diwan Athuman,Mkurugenzi wa Mashtaka,DPP Biswalo,E.Mganga na Mkurugenzi wa Upelelezi wa TAKUKURU, Alex Mfungo.-001Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Kamishna Diwani Athumani, Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Biswalo Mganga na Mkurugenzi wa Upelelezi wa TAKUKURU, Alex Mfungo.
4.Mkutano na wanahabri ukiendelea.-001Mkutano na wanahabari ukiendelea.
5.Wanahabri wakichukua tukio hilo.-001Wanahabari wakiwa na zana zao za kazi.

IDARA ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini kwa kushirikina na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) amesema jeshi la polisi kikosi cha upelelezi wa uhalifu wa fedha na mali limekamilisha upelelezi wa kesi 23 ambazo ziliwasilishwa kwa DPP na kati ya hizo tatu zimetolewa uamuzi.

Akizungumza na wanahabari makao makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai DCI, Kamishna Diwan Athumani, amesema kesi nyingine ishirini zipo katika hatua ya maombi ya kupata amri ya mahakama ili mali husika ziweze kuzuiwa au kutaifishwa.
Kamishna Athumani amezitaja mali zinazohusiana na uchunguzi huo kuwa ni pamoja na nyumba, viwanja, magari, boti na fedha taslimu za watuhumiwa, akibainisha kuwa wahalifu hutumia majina ya wake zao, waume zao na hata watoto wao katika kuficha mali wanazozimiliki na wakati mwingine kutumia majina ya watu ambao hawapo kabisa ili kuendelea kufaidika na mali walizozipata kwa njia ya uhalifu au ufisadi.
Ametoa rai kwa wananchi kutojihusisha kwa njia yoyote ile kuficha umiliki wa mali ya mtu mwingine kwa kudanganywa au kurubuniwa kutumia jina lake kuonesha kuwa wao ndiyo wamiliki wa mali fulani wakati siyo kweli.
Alisisitiza kuwa kufanya hivyo ni kutenda kosa kama ilivyo kwa mtenda kosa wa mwanzo na hivyo kuhusishwa kama mhalifu.
Aliwahakikishia wananchi kuwa taarifa zao kuhusu suala hilo kwa polisi zitakuwa za siri na zitalindwa kwa mujibu wa sheria kwa kuwa wamesaidia kwa namna moja au nyingine wakati wa upelelezi na ufuatiliaji wa mali zinazohusiana na uhalifu.

Na Denis Mtima/GPL

Leave A Reply