Johari: Nyerere Ametustiri Msiba wa Seth
MUIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’ amesema anamshukuru mwigizaji mwenzake Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ kwani ndiye aliyefanya mambo makubwa katika msiba wa mwenzao Seth Bosco.
Johari alisema, ilifi ka mahali wakati wanaratibu msiba huo, mambo yalikuwa magumu lakini alipojitokeza Nyerere, mambo yalibadilika ghafla.
“Mungu ambariki Nyerere kwa kweli, watu wamekuwa wakimzulia mambo yao bila kujua umuhimu wake, kwa kweli ametubeba katika msiba huu tukaweza kupata fedha kwa wadau mbalimbali,” alisema Johari. Seth ambaye ni mdogo wa Kanumba alizikwa Jumatatu Desemba 9, 2019 katika makaburi ya Kinondoni.