The House of Favourite Newspapers

JPM: ‘Aliye Tayari Kumwaga Damu Mwambieni Amwage Mkojo’ – Video

RAIS Dkt. John Pombe magufuli amewataka wananchi wa Wilaya ya Bukombe mkoani Geita na Watazania wote kwa ujumla kuendelea kuitunza amani na utulivu wa nchi hii ili kila mmoja afanye kazi yake kwa amani na upendo.

 

Magufuli amesema hayo leo Jumatano, Novemba 27, 2019 wakati akiwa ziarani wilayani humo huku akitolea mfano baadhi ya nchi jirani zilizokumbwa na machafuko yaliyosababisha vifo vya wananchi wake na kushindwa kufanya shughuli za uchumi badala yake kuuwana wao kwa wao.

 

“Endeleeni kulinda amani ya nchi yetu, amani ni muhimu sana, ninyi ni mashahidi, majirani zetu walipoichezea amani yao mliona shida waliopata, msije mkadanganywa na mtu yeyote ambaye anaweza kusimama na kuwaambia tuko tayari kumwaga damu, mwambieni amwage hata mkojo tu, mtamuona kama atabaki pale.

 

“Ninachowaomba ndugu zangu ilindeni amani yetu, palipo na amani utafanya biashara, utachimba dhahabu na kuiuza, utalima, hata kama unaposa utaposa vizuri na kanisani au msikitini utakwenda vizuri, tunzeni amani yenu. Wapo watu wanaweza kutumiwa hata na mabeberu, madhara yake mtayaona wenyewe. 

 

“Nawaomba tusibaguane kwa makabila, dini wala vyama, mimi ni mtumishi wenu katika kupeleka maendeleo mbele. Tanzania ni tajiri unaweza kuchimba madini kwenye mtaro ukakuta dhahabu, Ulaya hakuna. Sisi tumependelewa mno na Mungu, ukienda ziwani samaki wapo, madini yapo kila aina, hili taifa tuliloachiwa na Baba wa Taifa tusilivuruge,” amesema Magufuli.

 

MSIKILIZE AKIZUNGUMZA

Comments are closed.