The House of Favourite Newspapers

JPM: Mnataka CCTV ya Bil. 8? Mambo ya Ndani Hamjanielewa- Video

RAIS John Magufuli leo Novemba 25, 2019 ameweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi makao makuu ya Uhamiaji katika eneo la National Capital City jijini Dodoma. Jengo hilo la ghorofa nane ujenzi wake ulianza Mei, 2019 na utakapomilika Novemba, 2020 utagharimu Sh bilioni 30.

 

“Mnajua msiwafanye watu wajinga kwa kutamka CCTV Camera ni kitu cha ajabu sana, Mimi nilifunga kwa milioni tatu, sasa hii CCTV Camera ya hapa mpaka bilioni  nane ikoje? Ninajua mmetumia terms zile za kisayansi ili kusudi mtengeneze hela.

 

“Hatuwezi kutumia biioni nane kwa ‘CCTV camera’ na milango ya kujifungua yenyewe kwani wanaoingia humo hawana mikono, wanashindwa kusukuma hadi wawekewe rimoti, na ikiharibika lazima tutoe fedha za kununua vingine, basi ingekuwa hata fedha ndogo. Hilo suala la bilioni nane nimelikataa tafuteni milango ya kusukuma mfanye mazoezi, kwani mnashindwa kusukuma mbona huko nyumbani mnasukuma vitu vingi tu.

 

“Eneo hili ilikuwa pajengwe mji wa Serikali lakini kwasababu Uhamiaji wanatoa huduma kwa wananchi na wananchi wengi wako katikati ya mji ndipo ikaamriwa ofisi yao ijengwe hapa kati ya mji, nimefurahi kuona majengo yameanza kujengwa. Idara ya uhamiaji mmeniomba mambo mengi ikiwamo Nyumba, ajira na kupandishwa vyeo nimekubali ila hili la kutumia Sh bilioni nane katika vifaa vya ulinzi nimelikataa, lazima tuambiane ukweli”

 

“Tuna wafungwa 18, 000 gerezani tungeleta hata wafungwa 200 tukawapa majembe wangefanya ‘Land scaping’ nimesikitika kuona tunatumia fedha milioni 400 kwa kazi ambayo wangefanya wafungwa wapo tu gerezani”

 

 

“Askari wa Uhamiaji wanaenda kukaa Nyumba ambazo zimejengwa na askari wenzao wa magereza hii ni aibu kuna wafungwa wamefungiwa tu huko vyumbani, hamuwezi kuwatumia hata kufyatua matofali. Mambo kama hayo yanisikitisha kuona watumishi wangu bado hawajanielewa na katika Wizara ambayo hawajanielewa ni Wizara ya Mambo ya Ndani, hii ni aibu hilo mlishughulikie sana, nimezungumza sana lakini bado hamnielewi

 

 

Hata hivyo, katika kuipongeza wizara hiyo, alisema: “Passport uliyoizindua ya Tanzania imeshinda tuzo ya ubora na usalama kwa mwaka 2019 katika mabara ya Ulaya, Mashariki ya Kati na Afrika.”

 

Comments are closed.